Home
»
LULU
»
KIVAZI CHA AJABU CHA LULU MICHAEL CHAZUA UTATA
Mavazi anayovaa msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu,’ sasa
yanamuweka matatani kufuatia hivi karibuni kushambuliwa kwa maneno
kutokana na kigauni cha kimitego alichokuwa amevaa.
Kigauni hicho ambacho juzikati alionekana nacho mitaa ya Sinza jijini
Dar kisha baadaye kukitupia mtandaoni, kimewafanya wengi wahoji
anakoelekea msanii huyo anayedai amebadilika.
“Hivi huyu ndiye anayesema amebadilika kweli kwa mavazi haya, mbona
anataka kuwapa wakati mgumu wanaume? Ndo ili iweje sasa, ama kweli
jasiri haachi asili,” alisema mdau mmoja baada ya kuiona picha hiyo.
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Lulu ili kujua sababu ya kuvaa mavazi hayo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.