Home » » Ndege ya Ethiopian Airlines yatekwa na Rubani wake, Abadili uelekeo na kutua Uswis ili kuomba hifadhi ya kisiasa

Ndege ya Ethiopian Airlines yatekwa na Rubani wake, Abadili uelekeo na kutua Uswis ili kuomba hifadhi ya kisiasa


Rubani msaidizi wa ndege ya Ethiopian Airlines iliyokuwa ikienda Roma toka Addis Ababa ameteka ndege hiyo mapema leo na kuilazimisha itue Geneva, Uswisi, polisi wameieleza AFP.
  
Rubabi huyo alitenda kitendo hicho cha ajabu kama njia ya kujaribu kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Uswisi. “Anadai anaishi kwa hofu nchini kwake mwenyewe, hivyo anataka hifadhi Uswisi,” vyanzo vya kipolisi vimeiambia AFP.
 
Tukio lilivyotokea
Wanausalama Geneva wanasema rubani huyo msaidizi alivizia mwenzake alipokuwa amekwenda kujisaidia, kisha akajifungia katika chumba maalum cha kuongoza ndege na kubadili uelekeo wa chombo hicho kukipeleka Uswisi.
 
Baada ya hapo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni raia wa Ethiopia aliomba idhini ya kutua Geneva akidai anahitaji mafuta ya dharura. “Ghafla, akatutangazia kuwa ameteka ndege,” vimesema vyanzo hivyo.
 
Safari zasimama, huduma zavurugika
Kutokana na hati hati hiyo, ilibidi safari zote kuingia na kutoka uwanjani hapo zisitishwe mapema leo. Hata hivyo, kufikia saa 2:45 asubuhi kwa saa za ulaya ya kati, hali ya utulivu ilishaanza kurejea.
 
Polisi wamemtia ndani mteka ndege huyo, ambaye anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu ijayo, zasema taarifa zilizoifikia AF

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger