Home » , » JE WAUJUA UKWELI JUU YA KUFUNGIWA KWA VIDEO YA SNURA "NIMEVURUGWA" NA VIDEO YA JUX....!! BASATA WAELEZA SABABU...

JE WAUJUA UKWELI JUU YA KUFUNGIWA KWA VIDEO YA SNURA "NIMEVURUGWA" NA VIDEO YA JUX....!! BASATA WAELEZA SABABU...

Siku kadhaa zilizopita kupitia millardayo.com kuna taarifa ziliztoka kuhusu kufungiwa kwa video ya Nimevurugwa ya Snura,taaarifa hizi alizi-amplify meneja wake Snura ‘Hk’ akidai kuwa sababu maalum bado hawajazipata ingawa kila kituo anachoenda wanampa sababu tofauti.


Millardayo.com haikuishia hapo ilienda moja kwa moja kwenye Baraza la Sanaa la Taifa(Basata)ili kuujua undani wa sakata hili ikiwemo pia kuulizia video ya Jux(uzuri wako)ambayo nayo ilitoka taarifa ya kufungiwa kwa video hiyo.


Kutoka Basata huyu hapa Godfrey mungeleza ni kaimu katibu mtendaji  anataarifa zaidi>>Unaposema kufungia video moja kwa moja kuna chombo kingine cha serikali kinashughulikia hilo ambao ni bodi ya filamu Tanzania’




‘Bodi ya filamu wanaangalia video zote suala zima la filamu wanapoona hii haikidhi au haifai kwa jamii za Kitanzania basi wanaisimamisha kidogo wanamshauri aweze kuirekebisha ili iweze kulingana na maadili ya kitanzania’




‘Sisi tunaangalia Audio kabla haijaingia sokoni katika urasimishaji tunakaa tunausikiliza muziki wake tunashauriana kwamba akarekebishe hapa na tunaangalia mambo mengi ikiwemo ubunifu wake mwenyewe’


‘Suala la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la maadili na limeandikwa sana na sisi Baraza kama Baraza tunaangalia sana suala la maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia msanii mwenyewe’

Bonyeza play kumsikiliza Kaimu Katibu mkuu akielezea suala hili.


 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger