Msanii
wa filamu za Kibongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ amewapa makavu
laivu baadhi ya watu wanaoshangaa na kuhoji inakuwaje anatimiza mwaka
mmoja ndani ya ndoa bila kuzaa.
Akizungumzia
maneno ambayo amekuwa akiyasikia kutoka hata kwa watu wake wa karibu
wakiwemo wasanii wenzake, Jack alisema anawashangaa kwa kuwa wanashindwa
kujua kwamba kuolewa ni sheria lakini kuzaa ni majaliwa.