Home » » Mzee Mwinyi ndo mgeni Rasmi wa sherehe za Maulid katika mkoa wa Dar es Salaam....Kitaifa, sherehe hizo zinafanyika Kigoma ambapo mgeni rasmi ni Rais Kikwete

Mzee Mwinyi ndo mgeni Rasmi wa sherehe za Maulid katika mkoa wa Dar es Salaam....Kitaifa, sherehe hizo zinafanyika Kigoma ambapo mgeni rasmi ni Rais Kikwete



RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi leo atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za Maulidi Kimkoa, Dar es Salaam zinazofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 
Sikukuu ya Maulid inaadhimishwa na waumini wa dini ya Kiislamu duniani kote, ikiwa na maana ya kumbukumbu kuzaliwa kwa Mtume Muhamad(S.A.W).
 
Kitaifa, sherehe hizo zinafanyika Kigoma na mgeni rasmi ni Rais Jakaya Kikwete. Akizungumzia sherehe hizo, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salumu alisema zinaanza saa 2 leo usiku.
 
Alisema zinatanguliwa na maandamano ya dini, yatakayopita mitaa mbalimbali ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuelekea katika viwanja hivyo. Ujumbe wa Maulid ya mwaka huu ni ' Uislam kwa amani ya wote', ukilenga kujulisha kuwa misingi ya dini hiyo ni amani.
 
Kwa upande wake, Peti Siyame wa Sumbawanga anaripoti kuwa wakazi wa mkoani Rukwa, wanatarajia kujiunga na Waislamu duniani kote kusherehekea Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad katika mkesha ya maadhimisho hayo kwenye Msikiti wa Masjid Nuru.
 
Kwa mujibu wa Shehe wa Mkoa wa Rukwa ,Rashid Akilimali, mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Iddy Kimanta. Shehe Akilimali alisema wageni kutoka ndani na nje ya mkoa, wanatarajiwa kuhudhuria akiwemo, Naibu Katibu Mkuu Taasisi ya Tablidh, Shehe Amir Lulu akitoka jijini Dar es Salaam.
 
“Kuanzia kesho (leo) tunatarajia wageni kutoka wilaya zote mkoani hapa ikiwemo kutoka maeneo ya Kirando (Nkasi ) , Kasanga (Kalambo) mwambao mwa Ziwa Tanganyika kuanza kuwasili mjini hapa kwa ajili ya maadhimisho haya,” alisema.

 >>Habari leo
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger