Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni Yeuri (17 ), Gabriel (11) na Daniu RamÃrez (12), hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo.
Baba
yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia
televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa
wakiishi katika mateso kwenye jamii yao.
Baada
ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya Marcelino Velez Santana
nchini humo, Dokta Pedro Antonio Delgado aliamua kuwalipia gharama za
upasuaji ambao ulichukua saa mbili.
Ramirez,
alisema: “Wakati wanaingizwa katika chumba cha upasuaji nilikosa raha
kwa kuhofia kama watatoka salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka,
wote tumefurahi sana.”