Alisema kwamba baadhi wa wachekeshaji wanamchukiza kwa kufanya mambo ya aibu na kujidhalilisha wenyewe, badala ya kuchekesha akiwataka wajipange kabla kuvamia fani hiyo.
“Wapo vijana wanafanya kitu ukiangalia unafurahi na kwa sisi wachekeshaji wa siku nyingi unajifunza kitu, lakini hawa wavamizi ukiangalia unaweza kutapika. Sipendi na wananiudhi. Kama vipi wajipange upya,”alisema Majuto bila kuwataja akieleza kuwa anaowakusudia wanajijua.
Aliongeza kuwa kila kazi inahitaji umakini ili iweze kuvutia na kupata soko, akilalamika kwamba wachekeshaji wanaofanya kazi hiyo ili mradi wapate fedha ya siku wanawaharibia wenzao wanaotegemea kazi hiyo kwa maisha yao yote.
Alibainisha kuwa binafsi amefanya kazi ya uchekeshaji kwa zaidi ya miaka 55 na ndiyo inayompa heshima maishani mwake.