Kupitia Facebook, Madam Rita amewashauri wasichana wanaojikuta katika katika hali hiyo kutokata tamaa kwakuwa bado wanaweza kufanikiwa.
“Jambo mmoja msilofahamu kuhusu mimi,Nilipata ujauzito nikiwa na umri mdogo sana. Kwa jamii yetu inayotuzunguka, ukizaa katika umri mdogo, watu huwa wanakunyanyapaa, hukuona haufai kuwa katika jamii na hata kukuhukumu. Kwa umri ule niliona ni kama hamna tena maisha kwangu lakini sikukata tamaa na leo hii ujasiri wangu na kitu kinachonipa msukumo wa maisha hadi kufika hapa nilipo ni hicho kilichonikuta nikiwa na umri mdogo.Kukataa tamaa isiwe ndio chaguo lako la kwanza,” aliandika Rita.