Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omary Kopa amevamiwa na vijana wahuni wakitaka kumfanyia fujo kwa madai ya kukatiza mitaani akiwa ameongozana na ‘mwaume aliyekuwa amevaa nguo za kike’.
Tukio hilo lilijiri maeneo ya Kariakoo, Dar wiki iliyopita ambapo
vijana hao walianza kwa kuzomea wakitaka kumshika mwanaume huyo
waliyedai alikuwa amevaa nguo za jinsia ya kike.
Alichokifanya Khadija ni kuingia kwenye gari na kumwambia dereva
aondoke haraka kukwepa kufanyiwa vurugu huku mwanaume huyo naye
akiungana na malkia huyo kuondoka eneo hilo.
Wakizungumza na GPL, vijana hao walidai kuwa Khadija alijiabisha kwa kuongozana na mwanaume huyo.
Khadija aliiambia GPL kuwa alishangazwa na tukio hilo
lililomkuta na kusema kuwa mwanaume aliyeongozana naye ni mwimbaji
mwenzake ambaye pia ni shemeji yake.
Alifunguka: “Hivi kuwa mwimba taarabu wa kiume ndiyo ushoga jamani?
Au kuvaa kaptura ya kitenge ni tatizo? Mbona alikuwa amevaa mavazi
mazuri tu ya kiume?”
Khadija alisema kuwa amewazoea mashabiki wake wa Kariakoo kwani huwa
wakiwaona mastaa huwa na tabia hiyo na ndiyo maana walianza uzushi huku
wakisema kuwa waimba taarabu wote ni wanawake, kitu ambacho si kweli.
“Sikuona sababu ya kuchukua hatua, nilikuwa najaribu kuwaelewesha
lakini hawakunielewa, wakazidi kuzomea na kutuzingira ndiyo maana
tuliamua kuondoka,” alisema Khadija.
-Gpl
-Gpl