Diamond Platnumz ni bingwa wa kuitumia karata yake ya Public Relations vizuri. Mwezi August mwaka huu aliicheza vizuri baada ya kumfanyia surprise mwanamuziki mkongwe wa Tanzania Muhidin Gurumo kwa kumnunulia gari kwenye uzinduzi wa video yake ya 'My Number One' uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Jumatano hii, staa huyo aliyekuwa ameandaa show maalum ya Christmas
kwaajili ya watoto kwenye viwanja vya Leaders Club, alitisha tena baada
ya kuahidi kuwasomesha bure watoto watatu walioshinda shindano la
kucheza mtindo wake wa Ngololo.
"Management yangu ya WCB itawasomesha miaka yote waliyobakiza shuleni
ikiwa ni pamoja na kuwahamishia katika shule zilizo bora
zaidi,"aliandika Diamond kwenye website yake.