Maisha yalizidi kuwa magumu na sikuwa na jinsi zaidi ya kusafiri kutoka Moshi na kwenda kusini mwa tanzania kusaka maisha.
Tangu
mzee afariki maisha yalikuwa magumu kwetu na kama ujuavyo maisha ya
mama zetu wa kiafrika, baba zetu waliwasahau katika kuwaweka karibu na
utafutaji wa fedha wao walibaki nyumbani sasa fikiri mzee kafariki na
tuko watoto sita tutaishije?
Mama
yangu nilimwahidi lazima kabla ya uzee wake au kifo kumchukua lazima
afurahie matunda yake kupitia mimi na alikuwa na furaha kila siku kusia
maneno hayo toka kwangu.
Nilifika
mkoa huo kusini mwa Tanzania na nilishangazwa kuona mtoto mdogo kuliko
mimi ana utajiri wa kutisha.... duuuh mate yalikuwa yakinidondoka hasa
ukizingatia sikuwa na kipato cha kuanza biashara yangu wala elimu kubwa
ikabidi yule kijana aniajiri katika shamba lake la chai na mimi nikawa
msimamizi pale.
Baada
ya mwaka mmoja wa kuzoea pale huku nikifanikiwa kupata hela kidogo na
kumtumia mama yangu niaanza kuona mambo sio mabaya sana ila nakumbuka
kuna jamaa yangu mmoja aliyekuja nyuma yangu ghafla nikaanza kusikia
kuwa jamaa kashapata utajiri maana mara ananunua viwanja anajenga hotel
na fedha kibao. Ndipo nikaambiwa kuwa mimi tuu ndio fala wenzangu wote
huenda kijiji jirani ambako kuna mzee mmoja ambaye yeye huwapa vijana
utajiri.
Kwa
siri nikajiandaa na nikamtembelea yule mganga na hakuniambia nimpe hela
alisema ananipa dawa nikishapata fedha niende kumshukuru. Ila akasema
nilale pale kwani kuna mtihani nitaufanya kabla ya kwenda kuitumia ile
dawa na kuniuliza kama sio mwoga na nipo jasiri.
Jioni
ile alinipa mkuki na kuniambia nipite uchochoro mmoja na kuwa
nitakutana na kitu cha kutisha nisikiogope na nikienda hatua chache
nitakutana na cha pili wala nisiogope pia ila cha tatu tu kikitokea
niurushe mmkuki na kukiua pale pale kisha nirudi haraka kwa mganga.
Nikauchukua
mkuki na kuanza kuufuta ule uchochoro, hatua chache tuu nikaona bonge
la nyoka likinijia kwa mbele nikajikaza nae akasepa zake wakati huo
mkojo na jasho ninaninyanyasa, hatua chache mbele akatokea simba wa
ajabu nae ananifuata nikajikaza akapita na kupotea ile najiandaa kuuweka
mkuki sawa ili kile cha tatu nikipe mkuki mara naona mama yangu ndio
anakuja, niliutupa mkuki na kwenda kwa mganga na kumwambia aisee
nimeshindwa mimi plz nipe jaribio jingine hili la mama sio.
Mganga
akachukia na kunipa ndoano pamoja na fimbo yake na kusema nenda hapo
mtoni iinginze hii kwenye maji kitu ukihiisi kama samaki kimenasa wewe
ibebe ndoano na bila kuangalia nileteee.
Nikafanya
hivyo na ile ndoano ilivyokuwa nzito nikainyanyua na kuiweka mgongoni
na kisha kuondoka ila kabla sijafika kwa mganga nikasema ngoja nigeuke
na kuangalia ni nini, duuuh kumbe tena nimemvua mama yangu.
Nikakimbia
na kumwambia mganga mie nimeshindwa huku nikiwa nimechanganyikiwa
akanipa dawa na kusema kimbia sana tafuta usafiri uanze kwenda moshi
ukifika pale mmwagie mama yako maji haya.kwani muda huu atakuwa kaanguka
na wamemkimbiza hospitali maana utajiri huu ni lazima mama yako au
ndugu afe ili upate.
Niliunga
unga usafiri na siku ya pili jioni nikawa moshi, kweli wakaniambia mama
alianguka tu jana jioni na hawajui kuna nini, nikamwamgia dawa ile
akapona na ndio nikawasimulia kilichotokea.
Wakanisema
sana sana na sasa nimeokoka na nimepata utajiri kwa njia ya halali na
ninakoma na nimekoma kuupenda utajiri wa mkato…………….
credit--tabasamu na fuled