Home » » WANAFUNZI WANAOMUUNGA MKONO RAISI MORSI WAAMUA KUPAMBANA NA POLISI HUKO CAIRO..

WANAFUNZI WANAOMUUNGA MKONO RAISI MORSI WAAMUA KUPAMBANA NA POLISI HUKO CAIRO..

131006171033_cairo_clashes_ap_304x171_ap_nocredit_5d596.jpg

Polisi wa Misri wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga mkono rais wa zamani, Mohamed Morsi.
Mawe yalirushwa na pande zote mbili huku wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa, pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi miwili iliyopita.
Hii ni siku ya pili ya mapambano katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger