UHUSIANO wa wasanii wawili wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Geofrey Kusila umeota mbawa baada ya kumwagana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.
Chanzo kilicho karibu na wasanii hao kimepenyeza habari kuwa uhusiano wao umevunjika bila kufahamika chanzo.
“Nora na Geofrey wameshaachana na kila mtu ana maisha yake
hata kazi hawafanyi tena pamoja, tangu walipoachana Nora anaandaa
kipindi chake kwenye runinga na hayupo tena na Geofrey,” kilisema chanzo
hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Nora ili kuujua ukweli, akafunguka:
“Mimi ninafanya kazi zangu mwenyewe na Geofrey kivyake kwa
sababu tumeachana na kampuni ambayo tulikuwa tumeianzisha nayo imekufa
na baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake na kuangalia jinsi gani
atakavyofanya kazi hivyo hatupo pamoja tena.”