Home
»
KITAIFA
»
TANZANIA NA BURUNDI ZATENGWA TENA KATIKA MKUTANO WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)
NCHI za Tanzania na Burundi, kwa mara
nyingine zimetengwa na wenzao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ,
baada ya marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana mjini Kigali jana.
Marais hao walitarajia kujadili namna ya kuimarisha Jumuiya ya Afrika
Mashariki kupitia uimarishwaji wa miundombinu, uchumi, biashara pamoja
na kuweka mikakati ya shirikisho la kisiasa.
Kitendo cha Kutengwa kwa Tanzania na Burundi ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
kinazidi kutia shaka mtangamano wa jumuiya hiyo.
Nchi hizo mbili
zimeshaeleza kusikitishwa na muungano wa nchi hizo tatu, ambao zimesema
unakwenda kinyume cha makubaliano na mkataba wa EAC.
Katika
mkutano huo, marais hao, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa
Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, pamoja na mambo mengine, walitarajia
kusaini makubaliano ya kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya ushuru
kinachotarajia kurahisisha uchukuzi wa bidhaa kutoka Mombasa nchini
Kenya, Uganda hadi Rwanda.
Aidha Sudan Kusini ilialikwa ikiidhinishwa kama mshirika katika kikao hicho.
Mkutano
huo unakuja baada ya ule uliofanyika mjini Kampala, Uganda, Juni mwaka
huu na mwingine uliofanyika Mombasa, Agosti, ambako viongozi hao watatu
walipendekeza kupanuliwa kwa Bandari ya Mombasa, ili kuwezesha uharaka
wa bidhaa kupitishwa katika kuhudumia kanda nzima.
Mkutano
mwingine wa marais wa nchi 15 za Afrika, ikiwamo Tanzania, utafanyika
leo nchini hapa, katika kongamano la siku nne ambalo linatarajiwa kuweka
kipaumbele kwa uimarishwaji wa huduma za internet katika mataifa hayo.
Kwa
mujibu ya waandaaji, zaidi ya wajumbe 1,500 watahudhuria mkutano huo,
chini ya uenyeji wa Rais Paul Kagame na Dk. Hamadoun I. Toure, Katibu
Mkuu wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Kiteknolojia (ITU).