Home » » SAD: Watu Wawili wauawa kikatili..

SAD: Watu Wawili wauawa kikatili..

Watu wawili mkoani Shinyanga wameuawa kikatili mmoja kwa kuchomwa moto na mwingine kuchinjwa kama kuku.

Aliyechomwa moto anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 baada ya wananchi kumtuhumu kuiba kuku wanne.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga, Kamishina msaidizi wa polisi, Evarist Mangala, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa wananchi hao walimshambulia kijana huyo kwa kumpiga mawe, fimbo, marungu na kuuchoma mwili wake.

Katika tukio lingine Lucia Masunga (61), mkazi wa kata ya Kizumbi mjini hapa, aliuawa na watu wasiojulikana kwa kumchinja shingo na kusababisha kifo chake hapohapo.

Mwanamke huyo alivamiwa juzi majira ya saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake wakati akijiandaa kula chakula cha usiku na ndipo alipovamiwa na watu wasiojulikana na kisha kumchinja shingo na kusababisha kifo chake.

Kamanda Mangala alisema chanzo cha mauaji ya tukio la kwanza ni marehemu kutuhumiwa kuiba kuku na katika tukio la pili jeshi bado linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.

CHANZO: NIPASHE
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger