Home » , » MSANII WA BONGO MOVIE "IRENE PAUL" AMESEMA ATAOLEWA BILA MAHARI(BURE..)

MSANII WA BONGO MOVIE "IRENE PAUL" AMESEMA ATAOLEWA BILA MAHARI(BURE..)

MKALI wa sinema za Kibongo, Irene Paul amesema wakati wake wa kuolewa ukifika, hatatolewa mahari kama ilivyozoeleka badala yake atachukuliwa bila ya mume kugharamia.
Irene Paul.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Irene alisema linapokuja suala la kuolewa huwa haoni maana ya mahari kwani mahari inayotolewa haiwezi kufika hata theluthi ya malezi ambayo wazazi walimlea.
“Kama tumeafikiana kuoana na mchumba wangu sitahitaji mahari kabisa maana kwa upande mwingine naona kama ni kutugeuza kama watumwa sisi wanawake,” alisema Irene Paul.

-GPL
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger