Home » , » "DAVINA" AMESEMA HAHITAJI MARAFIKI...?? UNAJUA KWANINI KASEMA HIVYO,SOMA HAPA..

"DAVINA" AMESEMA HAHITAJI MARAFIKI...?? UNAJUA KWANINI KASEMA HIVYO,SOMA HAPA..

Nyota wa sinema za Kibogo, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kuwa hahitaji marafiki kwa sababu ni wasaliti hivyo urafiki wake mkubwa upo kwa wanawe.
Akichonga na paparazi wetu, Davina alisema tangu aingie kwenye ndoa amebadilisha mfumo wa maisha yake na kuwafanya watoto wake kuwa ndiyo marafiki zake kwani hawawezi kumsengenya wala kumsaliti kwa watu kama ilivyo tabia ya wengi.
“Mimi siku hizi sina marafiki kama ilivyokuwa zamani kwa
sababu kwanza sisi wasanii hatupendani na majungu ni mengi, unaweza kuongea na mtu jambo zuri lakini baadaye  ukaja kugeukwa na kuonekana mbaya, bora wanangu wawe marafiki zangu,” alisema Davina.
-GPL
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger