Home » » KUMEKUCHA..! Mataifa 10 Afrika yajipanga Kombe la Dunia Brazil 2014..!

KUMEKUCHA..! Mataifa 10 Afrika yajipanga Kombe la Dunia Brazil 2014..!


ShaJOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

WIKIENDI hii miamba 10 ya soka barani Afrika itaingia viwanjani kupambana kuwania nafasi tano za kuliwakilisha bara hilo katika fainali za Kombe la Dunia zilizopangwa kuchezwa Brazil mwakani.
Timu hizo ndizo zilizoingia raundi ya tatu ambayo ni hatua ya mtoano. Kivumbi kitakuwa leo Jumamosi na kesho Jumapili ambapo mechi za kwanza zitachezwa na marudiano yamepangwa kuwa kati ya Novemba 15 na 19.
Kila timu sasa ipo katika hatua ya mwisho ya maandalizi kwa ajili ya kujiandaa na mechi hizo ambazo zitachezwa nyumbani na ugenini. Washindi wa mechi hizo ndiyo watakaoiwakilisha Afrika katika fainali hizo maarufu duniani.
Wababe hao wanaowania fursa hiyo ni Ethiopia, Tunisia,  Ivory Coast, Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.
Kati ya hizo, Ethiopia na Burkina Faso ndizo ambazo hazijawahi kupata nafasi ya kuiwakilisha Afrika katika Kombe la Dunia.
Makala haya. inaziangalia mechi hizo kwa mtazamo ufuatao;
Ivory Coast v Senegal
Ivory Coast ‘The Elephants’ itaingia uwanjani Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan kupambana na Senegal ‘Lions of Teranga’. Ivory Coast imewahi kufuzu fainali hizo mara mbili wakati Senegal imewahi kufuzu mara moja tu.
Mechi baina ya timu hizo inatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa huku Ivory Coast ikipewa nafasi kwani kwa mara ya mwisho timu hizi zilipokutana katika mechi za kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa la Afrika za mapema mwaka huu, Ivory Coast ilishinda mabao 4-2 nyumbani.
Katika mechi ya marudiano jijini Dakar, Ivory Coast ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0 kabla ya mashabiki wa Senegal kuanzisha vurugu kubwa na hivyo mechi kuvunjika.
Kutokana na vurugu hizo, Senegal ilifungiwa kutumia uwanja wake wa nyumbani katika mechi za kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia. Kwa hiyo hata mechi ya marudiano dhidi ya Ivory Coast itachezwa kwenye uwanja huru.



 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger