Home » » JE UNAJUA CHA KUFANYA IKIWA MPENZI WAKO NI MWENYE HASIRA...?? SOMA HAPA...

JE UNAJUA CHA KUFANYA IKIWA MPENZI WAKO NI MWENYE HASIRA...?? SOMA HAPA...

Katika uhusiano wa aina yoyote, hakuna anayeweza kusema hajawahi kukasirika. Mara kwa mara tunakwazana na kukasirishana, lngawa wako wale ambao hasira yao iko karibu zaidi na huja kwa ukali zaidi na mara nyingine huleta madhara katika vitu, watu, au hisia za mpenzi mwingine. 
Hapa nataka nikusaidie jinsi ambavyo unaweza kufanya pale mpenzi wako anapowaka hasira kali. Kujua hili kutakusaidia kupooza au kuponya hasira za mwenzako na siyo kuchochea moto mkubwa zaidi ambao unaweza kuleta madhara makubwa zaidi.

Nini cha kufanya!
Ikubali hasira ya mwenzako kama ndiyo njia yake ya kuonyesha hisia zake.Hasira yake na kulipuka kwake kwaweza kuja kwa staili ya kuleta maudhi sana na wala kusikokuwa na sababu ya msingi, lakini kubali kuwa anahaki ya kuwa na hasira. Hasira yake yaweza isiwenzuri kwako lakini kumbuka haiashirii mwisho wa uhusiano wenu. Uhusiano uliyobora huruhusu kwa kiasi fulani vimikikimikiki kama hivi, huwezi kupinga visiwepo kwa asilimia 100.

Mfanye mpenzi wako kuwajibika kwa hasira yake mwenyewe
Najua anaweza kukulaumu wewe kwa hasira zake, iwapo hali hii inatokea kataa kukubali wazo hilo, wewe hauhusiki kwa chochote, wala wewe siyo sababu ya hasira hizo bila kujali yeye anasema nini.
Yeye ndiye amechagua kukasirika na kufanya hivyo anavyofanya, na mara nyingi ni mbinu yake ya kukufanya ukubaliane na matakwa yake. Kwa hali yoyote kataa kuchezewa kupitia hasira yake.

Tulia, na uwe na sababu ya kutulia kwako 
Hata kama mpenzi wako kavuka mipaka kwa kukutukana, kukulaani, kukupayukia au hata kukupiga, bado waweza kuchagua kuwa mpole na mwenye sababu maalum ya kutulia kwako. Taratibu na kwa upole mtulize kwa kumwonyesha uhalisia wa tukio. Kwa busara na kujizuia kwa hali ya juu, jitahidi kumweleza mawazo yako, hisia zako na ukionyesha jinsi hali hiyo inavyokusumbua mara inapotokea, kamwe usitumie sentensi za “wewe” mfano “wewe unaudhi sana”, “Wewe sikuelewi kabisa” bali tumia sentensi za “mimi”, mfano “mimi ninaumia sana unapofikia hali hii”. Endelea kutoa mawazo yako kwa ufasaha na katika hali ya kumjali.

Weka mipaka kwa hasira zisizo na sababu ya msingi
Kama mwenzako anazidi kuonyesha hasira yake isiyo na msingi, anatukana na kuendelea kubwatuka tu, na wala hakusikilizi unachotaka kukisema, basi unaweza kuamua kutoka na kuwa pembeni ya eneo hilo, kwa upole mwambie kuwa utafurahi kuzungumzia jambo hilo mara atakapopoa ukali na baada ya hapo nenda chumba kingine mpaka atulie.

Jizuie usiombe msamaha au kumtaka radhi
Najua watu wengi, hususan jinsia ya kike wakifikia hatua hii hujiona wao ndiyo wakosaji na hivyo kukimbilia kuomba radhi. Kumbuka kuwa mpenzi mkorofi, na mtukanaji hastahili kuombwa radhi. Nikweli yawezekana wewe ni sababu kwa kiasi fulani kwa tatizo hilo lakini kwa kule kukasirika kwa staili hiyo hakumfanyi astahili kuombwa radhi maana kwa kufanya hivyo utaendeleza tabia yake hiyo mbaya. Msamaha au radhi yaweza ikafaa baadaye kidogo wakati mpenzi wako ametulia na ameiweza hasira yake. Jaribu kuihifadhi samahani yako mpaka wakati huo ufike.

Mpongeze mpenzi wako mara tu anapoamua kufanya lile lenye staha na wala siyo anapoonyesha hasira.
Wakati wowote mpenzi wako anapoonyesha kushuka na kuelewa kuwa analofanya siyo jema, mpongeze, mtie moyo aendelee na tabia hiyo njema kwa kumwonyesha utayari wa kumsikiliza kile anachotaka kusema ili mfikie maafikiano.

Jipongeze pia
Kamwe usiruhusu matukano, kejeli na kashfa za mpenzi wako zikuvunje moyo na kukushusha thamani yako. Usijione mnyonge kwa lawama zake labda tu uchague kukubali anachokisema kwako. Jione bado kuwa wewe ni mwema na ulikuwa unafanya mambo kwa nia njema. Ukiweza jipongeze kwa kufanya kile ambacho hisia zako zitaona zimepongezwa. Mfano, jitoe mtoko, nenda kwenye filamu, jipikie kitu kizuri, fanya nafsi yako ijisikie iko juu.
Kama unajiona kuwa huwezi au unapata shida kuzifuata njia hizi basi jitahidi kumtafuta mshauri wa kisaikolojia (Counselor) kwa msaada zaidi.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger