Home » , » FAHAMU WALICHOANDIKA MASTAA WA FILAMU KATIKA KUMFARIJI WEMA SEPETU BAADA YA KUFIWA NA BABA YAKE MZAZI...!! Soma hapa ..

FAHAMU WALICHOANDIKA MASTAA WA FILAMU KATIKA KUMFARIJI WEMA SEPETU BAADA YA KUFIWA NA BABA YAKE MZAZI...!! Soma hapa ..

wema sepetu akiwa na mama yake pamoja na baba yake

Wema Sepetu yupo katika kipindi kigumu baada ya kuondokewa na baba yake mzazi balozi Abraham Isaac Sepetu aliyefariki leo hii. Mastaa wenzake hawakuwa nyuma kwa kumpa pole na kumfariji na baadhi yao ni hawa hapa



1.Mtunisy
Pole wema sepetu Kwa kuondokewa na Mzee wako Mungu akupe subra kipindi hiki kigumu inna lillah wainna illahi raajuun

2. Wastara 
Hakuna anayeweza kuzuia apangalo Molla chini ya jua, kifo kimeumbwa kwa ajili yetu sote tuko safarini ila tuko foleni siku ikifika lazima kwake urejee, pole Wema mungu akupe ujasiri wa kusimama pasi na baba ameen

3. Yobnesh Yusuph(Batuli)
Natoa pole zangu za dhati kwa familia nzima ya Mzee Sepetu, Mwenzezi Mungu awape moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amin Innalilah wainnailah rajooun

4.Salma Jabu Nisha
Pole sana mami.. Allah akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu ulichonacho.. cha kumpoteza baba yetu mpenzi Sepetu.. pole sana mama angu Allah yupo pamoja nanyi.. pamoja na sisi sote inshaallah.. #innalillahi wainnaillahi rajuun dad Wema Sepetu.

5.Elizabeth Michael(Lulu)
Pole sana mamie Wema Sepetu kwa kufiwa na baba yako, mwenyezi Mungu awape faraja na awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu, R.I.P baba yetu
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger