Home » » AFARIKI BAADA YA KUKOSA HEWA BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA...!

AFARIKI BAADA YA KUKOSA HEWA BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA...!



ITV imeshuhudia jitihada za jeshi la polisi na kikosi cha zimamoto na uokoaji wakishirikiana na wananchi katika kuondoa mwili wa marehemu ambapo wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamesema  marehemu alikuwa akichomelea vyuma ndani ya tenki hilo lililokuwa limeharibika ambapo gafla ulitokea mlipuko na kupelekea marehemu kukosa hewa ingawa  jitihada za kumtoa akiwa Hai zilishindikana kutokana na kukosa hewa.

Kwa upande wake mwakilishi wa zamu wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Morogoro Masoud Ramadhan amesema uchunguzi wa haraka uliofanyika umebaini  kuwa baada ya kutokea mlipuko uliosababishwa  harufu kali ya mafuta ndani ya tank hilo na ambapo mamehemu alikosa hewa

Mwili wa marehemu umechukuliwa na jeshi la polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Morogoro


 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger