JAMANI NITOKE NJE YA NDOA...?? NAHITAJI USHAURI WENU..

Nimevumilia majaribu ya ndoa yamenishinda, ninaishi na mke wangu lakini hatuna furaha yaani kama tumelazimishwa!

Hakuna kabisa furaha, tumejaribu kukaa chini na kujadili mara nyingi sana lakini huwa anadai hakuna tatizo! Najiuliza sana hivi kutoka nje ya ndoa kutanosaidia nini? Nitachinwa pesa bure na ndo matatizo yataongezeka lakini pia kiimani hairuhusiwi nami naogopa kukutwa katika dhambi na Mungu wangu!

Nimesali sana lakini kama hakuna badiliko lolote! Nimuache? Yaani kila kitu tabu tupu! Wasichana nawaogopa mno nahisi wataniongeza machungu je, nitamfute mmama wa wastani kama miaka 34 ila awe mzuri? mi nina 25. Kwakweli sijitambui niko njia panda!

Nilikuwa mwajiriwa wa kampuni fulani na nilikuwa nikilipwa laki 5 kwa mwezi sasa nina miezi 2 nkmeacha kazi sababu ya matatizo ya ndoa yangu!

Sijielewi nahisi naelekea kufa ningepata mwanamke wa umri huo na anaishi tofauti na.mji wangu na akanipenda ningeenda kukaa kwake hata kwa miezi 3.
Nahisi maisha yangu yanaharibika sasa,

Nina uchungu sana usiku huu nilikuwa safari nimerudi na zawadi zimepokelewa na kutupwa sitting rum, ninahamu nimemsogelea kitandani kanipiga pepisi jichoni nomeumia sana maana tangu tuoane sijawahi ifurahia ndoa!

Hapa najiuliza nifanyeje napanga nitoke nikalale guest lakini sina hata wakunifariji natoka naenda guest hata nikifika nikaamua kujitoa duniani inatosha.

Kuna wanawake wazuri sana, wapoleee sauti za upole akikukosea kidogo tu utasikia samahani baba yangu, nakupenda haikuwa nia yangu, jaman namimi si nipate mmoja wa hivi?


PICHA 5 : RONALDO APIGA PICHA ZA NUSU UCHI KWASABABU YA MBUNIFU GIORGIO ARMANI


 
Kutoka Majuu uko Tunamwangazia Mchezaji Mpira Maarufu  Duniani na mwenye Bei ghali kuliko wachezaji mpira wote Duniani namzungumzia  Cristiano Ronaldo mchezaji wa Real Madrid ya Uhispania lakini hapa tunaangazia kwenye maswala
 ya yeye kujiingizia pesa kama staa duniani.....Akiwa na umri wa miaka 25Cristiano  Ronaldo usiku wa Kuamkia
siku chache zilizo pita ameweza kumwaga wino wa Mkataba wa kupiga picha  na  Mbunifu Giorgio Armani mbunifu toka Italia wa kutangaza nguo za ndani kwa wanaume  na suruali aina ya jeans  za mbunifu huyo.....
Unajua hii imetokanaje!? kutokana na Ronaldo ni mchezaji  maarufu na mzuri duniani
so ameamua kumtumia kutangaza biashara yake akijua fika  shabiki yoyote wa Ronaldo akiona Ronaldo anazitanga ni lazima atanunua yule shabiki  wa Staa huyo duniani.... Giorgio Armani ameweza kumpa Ronaldo dola za kimarekani
 Milioni 20 kwa Kutangaza  Nguo hiyo ya ndani na Jeans hiyo na hapa meamua kukuwekea picha hizi uweze kuona taswira ya  kile nachokizungumzia....!1 Hongera kwa Staa huyo kuvuta mkwanja mwingi kwa kazi hiyo...!! Boxer hizo na jeans hizo zitaanza kuwa kwenye store mnamo tarehe 6.8.2014 kwa gharama ya boxer dola $98 na  jeans kwa dola $240 sawa sawa na boxer kwa pesa taslimu ya kitanzania itauzwa kwa 142,000/= na jeans itauzwa kwa Tsh 366,000

BABY MADAHA: SHILOLE NI MCHEZA VIGODORO TU, HANIWEZI KWA LOLOTE..

MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Madaha’ amemchana staa mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumwambia ni mcheza muziki wa uswahilini (vigodoro).
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Kauli hiyo ya msanii huyo anayetamba na Wimbo wa Summer Holyday, ameitoa siku chache baada Shilole kutema cheche zake kuwa Madaha aache kumfuatilia kwani amekuwa akiingia kwenye anga zake mara kwa mara.
Baby Joseph ‘Madaha’.
“Hivi huyu ana akili au matope, nimfuatefuate ana nini? Hebu aangalie muziki wangu ninaopiga na wake. Yeye ni wa hapa hapa, mcheza vigodoro,” alifunguka Madaha.

POLISI WATOA UFAFANUZI JUU YA MILIPUKO YA MABOMU ILIYOTOKEA ZANZIBAR..

JESHI la Polisi Zanzibar, jana limetoa ufafanuzi wa matukio ya milipuko iliyotokea katika maeneo manne tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Hamdani Omari Makame, alisema tukio la kwanza lilitokea Februari 23 mwaka huu, saa saba mchana eneo la Pangawe.

Alisema mlipuko huo ulitokea baada ya waumini wa dhehebu la Evengilistic kumaliza ibada na haukuleta madhara yoyote.

Aliongeza kuwa, wakati polisi wakishughulikia tukio hilo, saa 6:36 mchana ikatokea milipuko mingine mitatu katika maeneo mawili tofauti.

"Mlipuko wa kwanza ulitokea eneo la Malindi mjini Zanzibar kwenye Mkahawa wa Mercury unaomilikiwa na Bw. Simai Mohammed Saidi (45) lakini haukuwa na madhara.

"Ilipofika saa 8:35 na 8:40 kwenye mtaro mmoja uliopo karibu na Mkunazini, eneo la Mji Mkongwe, Mjini Zanzibar ilitokea milipuko miwili iliyopishana kwa muda wa dakika chache," alisema.

Alisema milipuko hiyo pia haikuleta madhara kwa binadamu isipokuwa gari moja lenye namba Z.355 ET Harrier mali ya Bw. Mohammed Ibrahim Ali, lililoegeshwa karibu ya mtaro lilipata madhara kidogo kwa kutoboka bati upande wa nyuma kulia.

Kamishna Makame alisema milipuko yote ilitengenezwa kienyeji na Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamechukua mabaki ya milipuko hiyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitaalamu.

Aliongeza kuwa, polisi wameimarisha doria katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Zanzibar ili kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena na kuweza kuwakamata wahalifu hao.

"Tayari timu ya Makachero wakiwemo Wataalamu wa Uchunguzi wa Kisayansi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi, Dar es Salaam, wamewasili mjini Zanzibar kuungana na Makachero wenzao wa Zanzibar kuendelea na uchunguzi huu," alisema.



Alisema katika hali isiyo ya kawaida, Mkoa wa Kusini Unguja, juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Unguja Ukuu, eneo la Kae Pwani, kulikuwa na wavuvi wakivua vyuma ili kwenda kutengeneza nanga ya boti lao, lakini wakati wakiendelea na kazi hiyo chuma walichokuwa wakikitengeneza kililipuka na kujeruhi watuwanne.

Waliojeruhiwa na kukimbizwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ni Juma Abdallah Juma (32), Shabani Khamisi Ibarahim (32) Haji Khamisi(35) na Sumai Hussein Hassan (38).


Wakati majeruhi hao wakiendelea na matibabu, majeruhi mmoja Juma Abdallah Juma (32) alifariki dunia saa 11 jioni na mmoja kati yao Sumai Hussein Hassani (38) alitibiwa na kuruhusiwa ambapo wengine wawili wanaendelea na matibabu.

MIMBA YA LINAH YACHOROPOKA.

SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, Amani limenyetishiwa kuwa ujauzito huo umechoropoka.
Astelinah Sanga ‘Linah’.
Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na kumfanya  Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.
“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.
Gazeti hili lilimtafuta Linah  kupitia simu yake ya kiganjani ili kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu kujitambulisha, staa huyo alikata simu.
Wiki iliyopita gazeti dada na hili, Risasi Mchanganyiko la Februari 19-21, mwaka huu liliandika habari za staa huyo kunasa  ujauzito  wa mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.
“Nani kakwambia kwamba nina  mimba? Hayo ni maneno ya watu, wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,” alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa

LAANA....!! PICHAZ ZA UTUPU ZA SUGARMUMMY ZASAMBAZWA MTANDAONI NA MPENZI WAKE...ZICHEKI HAPA....

BOFYA HAPO CHINI KUZIONA PICHA ZA UCHI ZA MDADA HUYO, NI KWA WAKUBWA TU...


EXCLUSIVE VIDEO YA PNC AKIMPIGIA MAGOTI NA KUTOA MACHOZI WAKATI AKIMUOMBA MSAMAHA USTAZ JUMA...

DIAMOND PLATNUMZ AWAJIA JUU WALE WANAOSEMA KAMPONDA ALI KIBA, SOMA HAPA ALICHOKISEMA...

Photo: kiukweli, nasikitishwa sana  jins baadhi ya wasanii kutwa  wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media, Mara sjui Nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"... sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi!

Kiukweli, nasikitishwa sana jins baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu, mara wengine wakizusha eti Nimewatusi kwenye Media, Mara sjui Nimepost kuwakashif, yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"... sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi!

-diamondplatnumz

Nesi Feki Anaswa Akiiba Kichanga Hospitalini… Apewa Kichapo na Kutembezwa Mtupu Barabarani

Nesi Feki

Nesi Feki Anaswa

Aibu Kubwa ya Kusikitisha, Kilichomkuta Dada Huyu Ama kwa hakika hawezi Kusahau Maishani Mwake . Nesi Feki  Ambaye Alinaswa Akiiba Mtoto Hospitalini Huko Nchini Ghana.
Tukio Hilo Lilitokea Wakati Dada huyo Alipoamua Kuvalia Sare za Hospitali kama Nesi na Kuamua Kuingia Wodi Ambayo Watoto Waliotoka Kuzaliwa Huhifadhiwa Kwa Muda kabla ya Kukabidhiwa kwa Mama zao.
Nesi Feki
Nesi Feki Anaswa Akitembezwa Mtupu
Baada ya Kufaulu Mtihani huo na Kuweza Kujipenyeza hadi kwenye Wodi Hiyo , Nesi Feki  Huyo Alimchukua Mmoja Kati ya Watoto Aliyeonekana Kuvtiwa nae na Kumficha Kwenye Begi Lake Akioekana kama Vile Amebeba Nguo.

Balaa Lamkuta

Balaa Lilimkuta Dada Huyo Kipindi Ambacho Alikuwa Akijaribu Kutoka Nje ya Hospitali Hiyo na Kwa Bahati Mbaya Mtoto Aliyekuwa Amemficha Ndani ya Begi Lake Akaanza Kulia Kwa Nguvu.

Mshangao

Walinzi wa Hospitali Ilibidi Kumzuia Kwa Muda Dada Huyo (Nesi Feki) Ili Kuweza Kumkagua na Kuona ni Kitu Gani Kilichopo Ndani ya Begi Alililokuwa Amelishikilia. Ndipo Kwa Mshangao Mkubwa Walinzi Walipomwona Mtoto huyo Mchanga Akiwa Ndani ya Begi Huku Akitapatapa Kutafuta Pumzi.

Atembezwa Mtupu

Wananchi wenye Hasira Kali Walianza Kumvamia kwa Kumpiga Bila Huruma na Kufanikiwa Kumvua Nguo zake na Kuanza Kumtembeza Barabarani. Hii Ni Aibu Kubwa Kuwahi Kuipata dada huyo Ambapo Wengi wamelihusisha Tukuio Hilo na Dhamira ya Kufanya Vitendo vya Kishirikina.

Kajala Aelezea Alivyonusurika Kifo baada ya Kunywa Kitu Chenye Sumu Hapo Jana.

Kajala
Kajala ni miongoni mwa waigizaji wa Tanzania ambao wamekua wakimake headlines mara kwa mara nchini Tanzania.
Screen Shot 2014-02-24 at 9.27.26 PM
Z

Wagoni Wapigwa Mawe hadi Kufa Huko Pakistan..

Wagoni

Wagoni Wauawa kwa Mawe.

Wagoni wawili Wanaokadiriwa kuwa na Miaka 30 kila mmoja Wameuwa Kikatili baada ya Kunaswa Wakishiriki Vitendo vya Ngono. Inasadikiwa Kuwa wagoni hao Kila mmoja na Ndoa yake na Kitendo cha Kunaswa Wakivunja Amri ya Sita Imewaghadhabisha Mno Raia wa Baluchistan Magharibi mwa Pakistan.
Aidha waliohusika na Mauaji ya Wagoni hao Wawili wamekamatwa na Polisi kwa Kosa la Mauaji, Baba na Kaka wa Mwanamke Pamoja na Mjomba wa Mwanaume wanashikiliwa na Polisi kwa Kosa Hilo la Mauaji.
Wagoni
Wagoni Wakiuawa kwa Kupigwa Mawe
“Ni kitendo cha Kikatili sana na Watu waliohusika na Mauaji haya ni Lazima Wafikishwe mbele ya Sheria” Alisema Bugti Ambaye ni Balozi wa Eneo Hilo la Magharibi mwa Pakistan

Hali ya Hatari.

Taarifa Zinaeleza Kuwa Kumekuwa na Ongezeko la Matendo ya Kinyama yanayofanyika Nchini Humo Hadi Kufikia Kiasi cha kesi 1000 kila Mwaka huku kukiwa na hofu ya Idadi Hiyo Kuzidi Kuongezeka Zaidi

MREMBO AFIA GESTI ARUSHA, CHANZO KIKIDAIWA KUWA USHIRIKINA...!! SOMA HAPA MKASA HUU...

MREMBO mmoja ambaye alihu-dumu kwenye nyumba ya kulala wageni na baa (jina tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Blandina Michael (33) amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba vya nyumba hiyo huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na vitendo vya ushirikiana.
Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara zake hupoteza maisha ghafla.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati alikanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa imani yake.
‘’Hao watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa ghafla kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila alimeza Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa kuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo hilo akihojiwa na polisi.
Marehemu Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi wake huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile alimwamini sana. Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la kiafya.
Bosi huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba hicho.
Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko wazi na alipochungulia alibaini kwamba Blandina alikuwa amefariki dunia.
Hata hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali mwili huo hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria kuuawa, ingawa mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.

HUYU NDIYE MZUNGU ALIYEKAMATWA NA KILO 5 ZA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR-ES-SALAAM

Raia wa Henellic, Alexamdrios Atanasios, amekamatwa maafisa wa usalama wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jumapili usiku Februari 24, 2014, akiwa na kilo tano za madawa ya kulevya.

Habari zinasema mzungu huyo alikamatwa wakati wa upekuzi, akijiandaa kupanda ndege ya Swiss air kueleke jijini  Zurich, Uswisi.
Madawa hayo yalikutwa yakiwa yamefichwa kwenye “sakafu” ya begi lake baada ya mitambo ya kisasasa yaupekuzi, kugundua kuwa kulikuwa na ‘mzigo’.
Habari zinasema, kwa sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwenye kituo cha polisi cha uwanjani hapo  akisubiri taratibu za kisheria ili afungukliwe mashtaka.

JE NINI HASA LENGO LA JIDE KUFANYA MAZOEZI YA KARATE...?? ANATAKA KUPIGANA NA NANI...?? HUYU HAPA MWENYEWE MSIKILIZE..


Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.


Itakuwaje Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama Shotokan, Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani hasa? Haya ni kati ya maswali ambayo wengi tulijiuliza.
Moko Biashara aka One B wa 100.5 Times Fm alimtafuta Lady Jay Dee na kutuwakilisha kwa kumuuliza maswali hayo nae akafunguka.
“Kwa sababu ninao muda wa ziada, halafu kukaa tu idol bila kufanya kitu saa zingine inaweza kupelekea mawazo yako kufikiria vitu vibaya. Kwa hiyo nikaona sio vibaya nikifanya mazoezi.” Alisema Lady Jay Dee aka Anaconda.
Alipoulizwa kama kuna mtu anataka kupigana naye alisema hakuna mtu ila anajiweka fiti tayari kwa lolote.
“Hapana ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio kwa ajili ya kutaka kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo likitokea ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza.
Mkali huyo wa Joto Hasira amedai kuwa ana mwalimu mzuri na kwamba yeye pia ni mwanafunzi mwenye bidii.
“Ni mwanzo tu lakini mimi mwenyewe ni mwanafunzi mwenye bidii, bidii yako pale ndio itakayokufanya uweze ku-improve kwa muda mfupi.” Lady Jay Dee alimwambia Moko Biashara aka One B.
Msikilize hapa:

PICHA: MSANII LULU WA BONGO MOVIE AAMUA KURUDI SHULE..

Kweli elimu ni  bahari na wala haina mwisho, picha aliyoipost kwenye mtandao hivi karibuni  wa kijamii inamuonesha msanii huyo mahiri wa bongo movie akiwa anapiga kitabu,huku wadau wakimuhasa apige kitabu uenda ikawa ni mkombozi wake

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger