Home » » MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AJINYONGA HUKO SHINYANGA KISA KIKIDAIWA KUWA MSONGO WA MAWAZO....

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AJINYONGA HUKO SHINYANGA KISA KIKIDAIWA KUWA MSONGO WA MAWAZO....


MWALIMU wa Shule ya Msingi Mwang’osha Kata ya Nyamalongo wilayani Shinyanga, Christipian Mafuru (24) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa madai ya msongo wa mawazo.
 
Mafuru ambaye alitumia kamba ya katani na kujinyonga kwenye choo chake. Ameacha ujumbe uliosomeka ‘Msongo wa mawazo umenilazimu nifanye hivi, poleni sana walimu wenzangu, samahani wazazi wangu, kwa heri mwanangu Ray.’
 
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Frida Maleko aliwaeleza waandishi wa habari kuwa waligundua mwili wake juzi saa 9:30 alasiri baada ya kutoonekana shuleni kwa muda mrefu.
 
Kwa mujibu wa Mwalimu Maleko, aliamua kumpigia Mwalimu Mafuru (marehemu) simu bila kupatikana na ndipo aliamua kwenda na walimu wenzake nyumbani, ambako mlango ulikuwa umefungwa huku simu ikiita.
 
Alisema hali hiyo iliwatia shaka, hivyo kuamua kuvunja dirisha la nyumba hiyo, ambako hawakukuta mtu, isipokuwa ujumbe huo ulioandikwa na kuachwa mezani. Mwalimu huyo aliajiriwa mwaka jana katika shule hiyo na alikuwa mchapakazi.
 
“Nilishituka kwa kutomwona muda mrefu shuleni, ikabidi nimpigie simu nimuulize kulikoni hujafika shule leo, lakini simu haikupokewa,”alisema Mwalimu Mkuu.
 
Baada ya kutomwona ndani, baadaye waligundua mwili wake ukiwa chooni.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangalla alithibitisha tukio hilo na kwamba chanzo cha kifo ni msongo wa mawazo na hiyo inatokana na ujumbe alioandika kwa mkono wake na kutia saini.
 
Alisisitiza hakuna mtu anayeshikiliwa na Polisi juu ya kifo hich

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger