Home » , » Mchungaji awaamuru waumini wake wale majani kama mbuzi ili waweze kuwa karibu na Mungu

Mchungaji awaamuru waumini wake wale majani kama mbuzi ili waweze kuwa karibu na Mungu



Umaskini, magonjwa na matatizo mengine yanayowakabili binadamu, yamewafanya waamini kila kitu wanachoambiwa na viongozi wao wa dini kama njia ya kuyaondoa.
Muumini akila majani ili kuwa karibu na Mungu Muumini akila majani ili kuwa karibu na Mungu
Mchungaji wa nchini Afrika Kusini amewafanya waumini wake wale majani kama mbuzi  eti ili waweze kuwa karibu na Mungu.
Mwanamke mmoja alidai kuwa kula majani kulimponya koo lake Mwanamke mmoja alidai kuwa kula majani kulimponya koo lake
Kwa maelekezo ya Pastor Lesego Daniel wa Rabboni Centre Ministries, mamia ya wafuasi wake walijimwaga kwenye uwanja nje ya kanisa lake kula majani huko Garankuwa, Kaskazini mwa Pretoria baada ya kuambiwa kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa karibu na Mungu.
Waumini wakiwa wamelala nje ya kanisa kula majani kama walivyoagizwa na mchungaji wao Waumini wakiwa wamelala nje ya kanisa kula majani kama walivyoagizwa na mchungaji wao
Mbinu hiyo yenye utata imekosolewa na watu wengi huku yeye akisema kuwa binadamu wanaweza kula chochote na wasidhurike. “Ndio tunakula majani na tunajivunia sababu inaonesha kuwa kwa nguvu ya Mungu, tunaweza kufanya lolote,” Rosemary Phetha aliliambia gazeti la Afrika Kusini la Times Live.
Kula majani kama mbuzi
Doreen Kgatle, 27, alipata kiharusi miaka miwili iliyopita anasema: Sikuweza kutembea lakini baada ya kula majani kama mchungaji alivyoagiza, nilianza kupata nguvu na saa moja baadaye niliweza kutembea tena.”
 
Picha zinazoonesha waumini mbalimbali wakila majani huku mchungaji huyu akiwakanyaga zimeleta mjadala mkubwa.
article-2537053-1A8B310100000578-989_306x423
Matokeo baada ya kula majani  ni kuumwa tumbo na kutapika
article-2537053-1A8B320400000578-643_306x423
Baada ya kula majani kilichofuata kilikuwa hiki
Times Live limeandika kuwa kwenye misa hiyo ya watu takriban 1,000 Daniel alisikika akisema ‘lala’ na watu sita wakalala usingizi. Aliwaagiza watu wengine kuwapiga vibao na kuwatikisa lakini watu hao walienda kulala bila kujitambua hadi pale alipowaagiza waamke.
1551669_711412385544134_1720454493_n
1497616_711412412210798_250937811_n
1507770_711412475544125_940043098_n
1526340_711413345544038_1450047438_n
‘Unaweza kuwaacha hivi kwa miezi sita. Naipenda hii. Sipendi kuboreka. Unaweza hata kuwafanya polisi wasinzie pindi wanapokuja kukukamata,” alisema.


>>Bongo5
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger