Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo haraka limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.
Mtendaji
mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo haraka Bi Asteria lambo amesema
basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye
uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya
150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salamu kuendelea kuwa na subira
na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua
mapema mwaka kesho.
Nao
baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea
kufurahishwa na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema
kama mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana
kutokana na adha kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo huku wakitoa wito
kwa mamlaka husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo
pindi yatakapoanza kufanya safari zao.
TIZAMA VIDEO HAPA..