Home » » Rais Kikwete awasili nchini akitokea ufaransa

Rais Kikwete awasili nchini akitokea ufaransa


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi akiwa njiani kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano unaohusu Amani na usalama na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Bara la Africa na Ufaransa.Kulia aliyesimama ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed na kushoto ni afisa itifaki.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Balozi Amina Mohamed wakati aliposimama kwa muda katika uwanja wa ndege jijini Nairobi, Kenya alipokuwa akirejea nyumbani akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano uliohusu Amani,Usalama na Ushirikiano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na bara la Afrika.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Mec Sadik akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi baada y kuwasili akitokea Paris Ufaransa ambapo alihudhuria Mkutano wa Amani,Usalama na Ushirikianokati ya Afrika na Ufaransa uliomalizika jana.
(picha na Freddy Maro)
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger