Home » » WATU WANNE WANAOHUSISHWA NA SHAMBULIO LA WESTGATE WAFIKISHWA MAHAKAMANI HUKO NCHINI KENYA..

WATU WANNE WANAOHUSISHWA NA SHAMBULIO LA WESTGATE WAFIKISHWA MAHAKAMANI HUKO NCHINI KENYA..


Wanaume wanne wamefikishwa mahakamani nchini Kenya baada ya kuhusishwa na shambulizi la kigaidi lililofanyika dhidi ya jengo la Westgate nchini Kenya mwezi Septemba mwaka huu.

Wanne hao wote walikanusha mashitaka hayo ikiwemo kosa la kuingia nchini bila vibali halali pamoja na kumiliki stakabadhi bandia za kujitambulisha. Mahakama imeamuru wawekwe rumande. Kundi la kigaidi la Somalia, Al Shabaab lilikiri kufanya shambulizi hilo la kigaidi ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa.

Wanne hao walishitakiwa kwa kosa la kuhusika na shambulizi hilo la kigaidi ingawa hakuna hata mmoja alikuwemo ndani ya Jengo la Westgate wakati wa shambulizi hilo.

Wanne hao raia wa Somalia ni Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Adan Adan na Hussein Hassan. Washukiwa hao ambao hawakuwa na mawakili walizuiliwa rumande kwa wiki moja baada ya kiongozi wa mashitaka kuomba muda zaidi kufanya uchunguzi.


 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger