Home » » WATU 6 MBARONI KWA KUMCHARANGA MAPANGA DKT MVUNGI ....VIDEO YA RIPOTI YA KAMANDA KOVA

WATU 6 MBARONI KWA KUMCHARANGA MAPANGA DKT MVUNGI ....VIDEO YA RIPOTI YA KAMANDA KOVA

WATU 6 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuhusika na tukio la kumshambulia Dkt. Sengondo Mvungi aliyevamiwa na majambazi nyumbani kwake Kibamba Msakuzi juzi. Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Selemani Kova amesema katika operesheni maalum iliyofanywa na jeshi la polisi, wamefanikiwa kuwakamata watu sita ambao majina yako yamehifadhiwa kwa sababu za usalama. Aidha Kamanda Kova aliongeeza kuwa bado hawajapata uthibitisho kamili juu ya sakata hilo na uchunguzi unaendelea kuwabaini wahusika halisi wa shambulio hilo

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger