Baadhi
ya Wataalamu wa kufichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ushirikina
na uchawi maarufu KAMCHAPE wamejikuta wakiwa kwenye mikono ya dola baada
ya kuendesha zoezi la kufichua uchawi katika nyumba kadhaa kwenye
vijiji mbalimbali vya manispaa ya Tabora ambapo baadhi ya wananchi
walililalamikia zoezi hilo kwa madai kwamba limekuwa likiwadharirisha
baadhi ya watu pamoja na kujenga chuki ambazo huenda zikasababisha
madhara makubwa katika jamii.
![](http://2.bp.blogspot.com/-uVRcwq_BmDg/UodffDHnjPI/AAAAAAAAm6M/b0WuQjCDa24/s640/1a.jpg)
Hapa
ni baada ya kufikishwa kituo kikubwa cha Polisi mjini Tabora kwa amri
ya Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya ambapo aliwataka kuacha
mara moja zoezi hilo la kufichua wachawi