Home » , » BONGO MUVI WAOMBWA KUMFARIJI WEMA SEPETU..!!!

BONGO MUVI WAOMBWA KUMFARIJI WEMA SEPETU..!!!

Watanzania hususan wadau wa burudani wameombwa kumpa sapoti mwigizaji na Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu katika kipindi kigumu alichonacho kufuatia kupata msiba wa baba yake mzazi,  Balozi Isaak Abraham Sepetu.

Meneja wa mwigizaji huyo, Martin Kadinda ameliambia Mwananchi kuwa ingekuwa vizuri zaidi kama washabiki na wapenzi wa burudani kwa jumla wakashirikiana naye katika kumpa sapoti mwigizaji huyo.

Wema anapitia kipindi kigumu sana, nafikiri kila mmoja wetu anaelewa uchungu wa kufiwa na mzazi. Naomba kwa niaba yake tuungane pamoja kumfariji yeye na familia yake ili waweze kupita salama katika kipindi hiki”, anasema Martin.

Baba wa Wema Sepetu  Balozi Isaac   Abraham Sepetu alifariki dunia  Jumapili wiki iliyopita katika Hospitali ya TMJ alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa kisukari pamoja kiharusi.

Balozi Sepetu alizikwa siku ya Jumatano Oktoba 30, 2013 kijiji cha Mbuzini, Mjini Magharibi Unguja.

Mwanamuziki Diamond ni kati ya walioshiriki msiba wa baba Wema, hali iliyosababisha baadhi ya watu kujiuliza kama wawili hao ambao waliwahi kuwa na uhusiano, wanarudiana au aliamua tu kuja kama walivyo watu wengine.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger