Home » » Sakata la mtanzania aliyefariki dunia baada ya kutandikwa risasi na polisi mkoani Tanga

Sakata la mtanzania aliyefariki dunia baada ya kutandikwa risasi na polisi mkoani Tanga



Mtu mmoja amefariki na mwingine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na Askari polisi wilayani Lushoto mkoani Tanga baada ya askari huyo kudai kujeruhiwa na watu hao kwa kukatwa mapanga manne katika kichwa chake na mkono wa kushoto.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Costantine Massawe amesema hili tukio limetokea saa nne na nusu  jana usiku kwenye kijiji cha Shume tarafa ya Mlola ambapo askari huyu aitwae Oforo, amejeruhiwa alipokwenda na wenzake wawili kumkamata mtuhumiwa kutokana na kibali kilichotolewa na Mahakama wilayani humo kufuatia mgogoro wa ardhi.

Walipofika, walitokea watu wawili waliowashambulia askari kwa mapanga kitendo kilichofanya askari huyu kuwafyatulia risasi na kumuua mmoja wao ambae alifariki akifanyiwa matibabu kwenye hospitali ya Lushoto huku aliejeruhiwa akiendelea kupata matibabu.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger