Home » , » MAPENZI YAMPOTEZA SKAINA..ASEMA WANAUME WOTE ANAOKUWA NAO WANAMKATAZA KUIGIZA...!!

MAPENZI YAMPOTEZA SKAINA..ASEMA WANAUME WOTE ANAOKUWA NAO WANAMKATAZA KUIGIZA...!!

STAA wa sinema za Kibongo, Skyner Ally ‘Skaina’ amepotea kwenye gemu chanzo kikidaiwa kuwa ni mapenzi kwani kila mwanaume anayeanzisha naye uhusiano wa kimapenzi, humzuia kuendelea kufanya kazi za sanaa.
‘Akibadilishana sentensi’ na mwandishi wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema kitendo cha wanaume wengi wanaoanzisha uhusiano na Skaina kumzuia kuendelea na kazi ya uigizaji, kimechangia kumpoteza.
Mwandishi wetu ‘alipomvutia waya’ Skaina, aliambulia majibu ya ‘sintofahamu’ huku akisisitiza kutosumbuliwa.
“Sasa kama umeambiwa hivyo mnachoniuliza hapo ni nini? Kwani lazima niigize mara kwa mara? Mimi naipenda kazi yangu, sitaki maswali zaidi,” alisema Skaina.
-risasi
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger