Home » » KOCHA MAN CITY ATAKA KUMNYOFOA VALENCIA MAN UNITED KWA PAUNI MILIONI 12.5 ...

KOCHA MAN CITY ATAKA KUMNYOFOA VALENCIA MAN UNITED KWA PAUNI MILIONI 12.5 ...

        KOCHA wa Galatasaray, Roberto Mancini anapanga kumchukua winga wa wapinzani wake wa zamani katika Jiji la Manchester, Antonio Valencia wa United.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester City anamataka mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ecuador kwa dau la Pauni Milioni 12.5 ili kuimarisha alichokirithi kwa Fatih Terim.
Kocha wa Old Trafford, David Moyes amemuondoa Valencia katika orodha ya wachezaji muhimu, na kuibuka kwa nyota kinda, Adnan Januzaj kumempunguzia nafasi katika kikosi cha kwanza.
New start: Galatasaray boss Roberto Mancini wants to sign Manchester United winger Antonio Valencia
Mwanzo mpya: Kocha wa Galatasaray, Roberto Mancini anataka kumsajili winga wa Manchester United, Antonio Valencia
Fighting fit: Valencia, (left) in training for Ecuador this week, has fallen down the pecking order at United
Anapambana kuwa fiti: Valencia, (kushoto) akiwa mazoezini na timu ya taifa ya Ecuador wiki hii, amepoteza nafasi kikosi cha kwanza cha United
Red Devil: Valencia (left) signed for United in 2009 from Wigan, but could now be on the move
Shetani Mwekundu: Valencia (kushoto) alisajiliwa United mwaka 2009 kutoka Wigan, lakini sasa anaweza akawa anachungulia mlango wa kutokea
Na sasa Valencia anaweza kupata nafasi Galatasaray, kwa mujibu wa gazeti la Uturuki, Fanatik.
Pamoja na hayo wanaweza kukabiliana na upinzani kutoka klabu ya zamani wa Moyes, Everton, ambayo inamtaka winga huyo kama sehemu ya dili ya kumuuza Leighton Baines Januari.
Dili litamaanisha kwamba Mancini atatakiwa kupunguza mchezaji wake mmoja wa kigeni katika kikosi cha sasa ili kuendana na sheria ya idadi ya wachezaji wa kigeni ya Shirikisho la Soka Uturuki.
Mshambuliaji wa zamani Chelsea, Didier Drogba kwa sasa anaongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ya Uturuki, na Mancini anataka kuweka alama yake katika kikosi hicho.
Through his paces: Everton could also make a move for Valencia in return for Leighton Baines, in England training
Everton inaweza kumtaka Valencia katika mauzo ya Leighton Baines,aliye mazoezini na kikosi cha England training
Starlet: Valencia's playing time has been reduced thanks to the emergence of Adnan Januzaj
Winga teleza: Nafasi ya Valencia katika kikosi cha kwanza United imepungua baada ya kuibuka kwa  Adnan Januzaj

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger