Home » , » "BADO HATUJAMFIKIA NYERERE KIUTAWALA BORA, TUNA MAPUNGUFU MENGI SANA"....BUTIKU

"BADO HATUJAMFIKIA NYERERE KIUTAWALA BORA, TUNA MAPUNGUFU MENGI SANA"....BUTIKU


Oktoba 14 ya kila mwaka imetengwa katika Tanzania kuwa siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Katika kukumbuka siku hiyo Mwandishi Wetu, Exuper Kachenje amefanya mahojiano na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Mwaka wa Mwalimu Nyerere kwa miaka mingi, ambapo anaeleza mambo mbalimbali kuhusu miaka 14 ya Tanzania bila kuwepo kwa kiongozi huyo.
Swali: Kwa miaka 14 tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, amefariki dunia, ukiwa mmoja wa watu waliokuwa karibu naye, ukiwa Katibu Myeka wake, Je, unahisi kukosa nini kutoka kwake?
Jibu: We, akitutoka baba yako inakuwaje? Akiondoka, kama binadamu unakosa mtu mwenye ubinadamu, aliyekuwa kiongozi wako na wewe msaidizi wake, unamkosa.
Kwangu, Nyerere alikuwa baba, mwalimu na  Baba wa Taifa. Tungefurahi kama angeendelea kuwa nasi leo hata kama angekuwa kikongwe kiasi gani au hana meno;
Ninakosa staili yake ya utendaji, uwezo wa kufikiri, kutenda, kueleza mambo kwa ufasaha na usahihi wa kiwango kikubwa. Hivyo, tunakosa mawazo ya msingi kama kuheshimu utu wa watu wote na usawa wa watu.
Swali: Binafsi umechota nini kutoka kwake na unakitumiaje?
Jibu: Nimechota uadilifu, ukweli, heshima kwa watu wote, kujali watu na kujitahidi kuwa mtu kwa watu wengine. Mwalimu alikuwa ‘role model’ (mtu wa mfano) wangu. Kitu ambacho sikuweza kuchota kutoka kwake, ni imani yake katika utu na usawa kwa wote, niliona imani hiyo na iliendana na imani yake katika kumcha Mungu na jitihada zake kuhudumia watu kadri ya imani yake ya Kikristo.  
Mwalimu alikuwa mtu mwenye kuona mbali, alipenda umoja, amani kubwa na ndogo, mwadilifu, mtu maalumu aliyetumia muda wake wote kutumikia watu wengine.
Tunaweza kusema, sisi tunajitahidi kufuata yake, lakini hatujamfikia bado tuna upungufu.
Swali: Unapozungumzia upungufu, unaitazamaje Tanzania ya leo ukiwianisha na mambo aliyoasisi?
Jibu: Yapo mengi mazuri yaliyoendelezwa na sisi tuliobaki na viongozi wetu, moja ni Utanzania umeendelezwa. Tumedumu kama Watanzania tukiwa wamoja na ukisikiliza Watanzania hao wanapenda taifa lao, wanapenda umoja wao, wanapenda amani yao, wanataka uhuru wao, wanapenda mali zao zikubalike na zitambuliwe kuwa zao.
Wanapenda viongozi wao wajue kwamba ni viongozi wa watu na wajali wananchi, lakini hatujawa na viwango vya kukosa amani na kuyumbisha nchi yetu.

MWANANCHI
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger