Home » , » AIBU...!!MCHUMBA WA MTU ANASWA LIVE AKIJIUZA...AZIMIA NA KUTOKWA MAPOVU BAADA YA KUNASWA KWA "KIMBOKA "

AIBU...!!MCHUMBA WA MTU ANASWA LIVE AKIJIUZA...AZIMIA NA KUTOKWA MAPOVU BAADA YA KUNASWA KWA "KIMBOKA "


Mchumba huyo wa mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Diva alitoa kali ya mwaka baada ya kuzimia ghafla huku akitokwa na mapovu kinywani baada ya kunaswa na OFM akijiuza.
Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita maeneo ya Kimboka, Buguruni, Dar ambapo msichana huyo pamoja na ‘madadapoa’ wenzake walikuwa wakifanya biashara hiyo haramu bila kificho.
Mara baada ya kuona wenzake wakiwa mikononi mwa nguvu za dola katika kamatakamata ya polisi, mrembo huyo ambaye baadaye alijitambulisha kama mchumba wa mtu, alianguka ghafla na kuzimia kiasi cha kuzua hofu miongoni mwa machangu wenzake walioangua kilio wakidhani mwenzao amekata ringi (kufa).
Baada ya muda msichana huyo alirejewa na fahamu akiwa mikononi mwa polisi na kuanza kuangua kilio akiomba asikamatwe kwa kuwa yeye ni mchumba wa mtu na atakuwa kwenye wakati mgumu kama mchumba’ke atajua anajiuza.

“Naomba msinikamate. Mimi ni mchumba wa mtu afande. Mtaniweka kwenye wakati mgumu kama akijua nilikuwa nikijiuza. Jamani nitamkosa mchumba wangu Luka,” alisema mrembo huyo huku akiomba maji ya kunywa.
Hata hivyo, kilio chake hakikuwazuia ‘OFM’ kufanya kazi yake ndani ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar  ambapo watuhumiwa hao wanasubiri kupandishwa kizimbani kwa ajili ya taratibu za kisheria.

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger