Siku chache baada ya staa wa Injili Bongo, Rose Muhando kudaiwa kutiwa mbaroni kwa utapeli wa shilingi milioni 6, nyuma ya skendo hiyo, mapya yameibuka.
Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella
Joel, mara kadhaa Rose alishaingia kwenye skendo nyingi kutokana na
jamaa aliyetajwa kwa jina la Nathan Wami.
Alisema katika albamu ya Rose ya kwanza kabisa iitwayo, Jipange
Sawasawa alijikuta akiingia kwenye balaa la kubambikiwa msala wa kudaiwa
kukutwa na madawa ya kulevya ambapo katika mazingira yeye utata, staa
huyo alijikuta akiziachia shilingi milioni 30 bila kujijua kwa baadhi ya
polisi wa Dodoma. Hiyo inadaiwa ilikuwa ‘karibisha mgeni’.
Stela
alifafanua kuwa, hata msala ambao ulimfikisha Rose korokoroni katika
Kituo cha Polisi cha Msimbazi Dar hivi karibuni siyo wa shilingi
milioni 6 kama
ilivyoelezwa awali bali ni sh. milioni 2 ambazo si yeye aliyezipokea
bali ni mwanaume huyo.
Alieleza kuwa katika msala huo wa milioni 2 alizodaiwa kuchukua na
kushindwa kwenda kufanya shoo Mombasa, Kenya, staa mwenzake wa Injili,
Jennifer Mgendi alidaiwa kujua kila kitu alikataa kwenda Msimbazi kumtoa
Rose akidai kuwa hajui chochote.
Stella alifunguka: “Tofauti na watu wanavyojua, Nathan hakuwahi kuwa
meneja wa Rose bali alikuwa ni msaidizi wake tu. Kwa hiyo si kweli
kusema eti Nathan aliamua kumwacha mwimbaji huyo kwa kisingizio cha
kukosa mwelekeo.
“Msada pekee wa Nathan kwa Rose ni kumlipia gharama za studio
alipokwenda kurekodi kwa mara ya kwanza wakati Rose akiwa anasali Kanisa
la Saint Mary, Chimuli, Dodoma. Ila kama mlivyiosema kwenye gaeri la
Ijumaa (Wikienda) kuna mengi yapo nyuma ya pazia.
“’Ukichaa’ wa Rose ni pale alipokosea akaenda na Nathan, Cosota
(chama cha hatimiliki) na kuingia makubaliano kwa maandishi kwamba huyo
Nathan ndiyo awe analipwa mrabaha (sehemu ya mapato) ya kazi zote za
Rose. Ni juzijuzi tu ndiyo Rose akaniagiza mimi nikamtengulie huo
mkataba,” alisema katibu huyo ambaye pia ni mwimba Injili.
Aliendelea kufafanua kuwa mikataba yote ya kazi za Rose alikuwa
akisaini Nathan hadi mwimbaji huyo alipochukuliwa na lebo kubwa ya Sony
inayosimamia kazi zake kwa sasa.
Akaongeza: “Kama pesa yote ingekuwa inaingia mikononi mwa Rose
asingekuwa hivi alivyop leo. Fikiria mpaka sasa Rose ana gari moja tu
(Toyota Prado), viwanja 3 na shamba la eka 100 pale Dumila, basi
(Morogoro).”
Kwa upande wake, Rose alisema kuwa Nathan alimfanya mashine ya kutoa na kuweka fedha benki (ATM).
Nathan alipoulizwa juu ya madai yote hayo alijibu kwa sauti yenye
uhakika: “Hayo madai si ya kweli. Mimi nimeishi na Rose kwa zaidi ya
miaka 12. Mimi ndiye niliyemsaidia yeye. Asingekuwa alivyo sasa kama si
mimi.”
>>Risasi Jumamosi/ GPL
>>Risasi Jumamosi/ GPL