Home » » "MASTAA WENGI WAMETOKEA KWENYE UCHANGUDOA NA KUVAMIA TASNIA YA FILAMU"...KAULI YAMPONZA DUDE...SOMA ZAIDI

"MASTAA WENGI WAMETOKEA KWENYE UCHANGUDOA NA KUVAMIA TASNIA YA FILAMU"...KAULI YAMPONZA DUDE...SOMA ZAIDI

WASANII wa kike wanaotamba kwenye filamu za Kibongo, hivi karibuni wamembwatukia staa mwenzao, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na kuipinga kauli yake kwamba mastaa wengi wa kike wametokea kwenye uchangudoa na kuvamia tasnia hiyo, shuka na mistari uipate habari hii.
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Wakizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamemtaka Dude kuacha tabia ya kuropoka kwani kauli yake imewavunjia heshima mbele ya jamii.
Baadhi ya mastaa waliotoa kauli za kumbwatukia Dude na kauli zao ziko hapa chini ni hawa wafuatao:
Tamrina Poshi ' Amanda".
TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
“ Ni heri Dude aache kuzungumza vitu visivyokuwa na maana, ajifunze  mambo mazuri kwani ni mtu mzima sasa. Kila mara anatuponda wasanii wa kike, kila mtu ana maisha yake kama wapo wanaofanya uchangudoa hao ni hulka zao, sina tabia hiyo na sanaa nimeianzia kwenye vikundi .”
Upendo Mushi 'Pendo'.
UPENDO MUSHI ‘PENDO’
“Kauli ya Dude siyo ya kweli kama wapo ni  baadhi na siyo wote, sijaingia kwenye sanaa kwa rushwa ya ngono na sina tabia hizo, sijaipenda kauli yake.”
BABY MADAHA
“Siyo kweli kwamba sisi ni machangudoa . Wasanii wa kike wenye tabia hizo wanatoka katika maisha duni na wale wanaolipwa malipo duni kwenye filamu lakini wengine tumetokea kwenye familia   za hadhi na tunaishi kwa kufuata maadili.”
HALIMA YAHAYA ‘DAVINA’
“Sijaipenda kauli ya Dude, ametukosea sana ingawa watu wengi wanaona tasnia hii ni kama  ya kihuni lakini siyo wote wenye tabia hizo za kihuni, wengine tunajiheshimu na tuna familia zetu tunaithamini sanaa  tunaichukulia kama kazi.”
SNURA MUSHI
“Dude ameongea uongo, binafsi siko hivyo na sina maisha ya kuzurura, starehe na pombe na sitarajii kuwa na maisha hayo, ili heshima yake iendelee, angetuomba radhi na kuifuta kauli yake.”
MIRIAMU JOLWA ‘JINI KABULA’
“Huo ni mtazamo wa Dude, wasanii wa kike tunatakiwa kumuombea kwa Mungu ili ampe akili za kuweza kuzungumza vitu vya maana na siyo hivyo vya kutushushia heshima kwenye jamii.” 

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger