Sasa baada ya kuacha biashara za familia mimi nikaanza biashara yangu mwenyewe pasipo kumwambia mume wangu, nimefanya kwa siri hiyo biashara na kwa kweli namshukuru Mungu inaenda vizuri kwani nilianza na mtaji mdogo lkn sasa nina turnover nzuri tu, kwa kweli namshukuru Mungu..
Sasa biashara imekua na wakati mwingine inanibidi kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya hiyo biashara yangu...nimeshafanya mara kadhaa lakni namdanganya naenda kikazi (nimeajiriwa pia) while in fact nasafiri kwa mambo yangu tu..
na hapo hapo nimeweza kununua plot 3 na nyingine moja nimeanza kujenga sijamwambia, kwani pesa hizo napata kwenye biashara yangu na yeye haijui hiyo biashara..na zenyewe hizo plot na nyumba nayojenga sijamwambia sababu naogopa nikimwambia ataanza kunihoji umepata wapi hela wakati nafanya biashara ambayo namshukuru Mungu kwa kweli inanilipa kdg, nilianza kama utani tu lakini inaenda vizuri..(sio sembe jamani) ni biashara ya kawaida tu ya kununua bidhaa na kuuza..
Pia nilinunua gari ambayo nilimdanganya nimekopa kazini lakni ukweli sijakopa popote, nimenunua tu kwa vihela vya mshahara pamoja na faida kutokana na hiyo biashara nayofanya..
Sasa nifanyeje ndugu zangu, nimwambie mume wangu au niendelee kuuchuna tu? naogopa nikimwambia ataanza yale yale ya kukopa hela halafu harudishi...kwa ujumla hana discpline na hela, ana matumizi mabaya na huwa anaishiwa na kuanza kukopakopa watu, kitu ambacho nimemdhibiti lkn nimeshindwa..
Naogopa nikifa leo sijui itakuwaje, huyu ninayefanya nae biashara hatanidhulumu? (kuna mtu nimemuajiri, tunaelewana sana, lkn hajui km mume wangu hajui kwani sijamwambia hayo,)...watoto wangu sio wakubwa wa kuwashirikisha vitu km hivyo kwa hivo hawajui..
Lakini nimemwambia kaka yangu na nimeandika usia, na pia kaka yangu anajua hizo plot zote nilizonunua na nyumba ninayojenga, nimemuonyesha na nimemwambia kabisa kuwa shemeji yako(yaani mume wangu) hajui...nina dada yangu ambaye ningeweza kumwambia na yeye lkn si mtu mwenye kutunza siri anaweza akaropoka ikawa tabu kwa hivo sijamwambia..
jamani wadau niko sawa au? hebu nisaidieni mawazo