Wananchi 6,700 wa Kata ya Kilolambwani wilayani hapa wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa chakula na kusababisha baadhi ya wananchi kula mizizi ya porini.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata
hiyo, Salamu Matajabu pamoja na wenyeviti wa Serikali za Vijiji vya
Nangole na Dimba wakati walipokuwa wanazungumza na timu ya waandishi wa
habari kwa nyakati tofauti mjini Lindi jana.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Dimba, Abdalla Mbwana amesema hali ya chakula kwa wananchi wake ni mbaya
jambo linaloweza kusababisha baadhi ya wakazi wa kijiji hicho kupoteza
maisha kutokana na kukosa chakula.
Naye Diwani wa kata ya Kilolambwani
Salamu Mtajabu alisema tatizo la njaa katika eneo hilo limevikumba
vijiji saba vinavyounda kata hiyo lililosababishwa na ukosefu wa mvua
kwa misimu miwili mfululizo wa 2010/11 na 2012/13.
Matajabu alisema zinahitajika juhudi za
makusudi na haraka kuwapatia msaada wa chakula wananchi hao ili kuokoa
maisha ya wakazi hao .
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Lindi,
Dk Nasoro Himidi alisema tatizo la upungufu wa chakula katika kata hiyo,
ofisi yake inalitambua na tayari ameomba tani 19,000 za nafaka Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa .
Hata hivyo katika utafiti wa hivi
karibuni imebainika kuwa takribani wa watu Milioni 840 wanakabiliwa na
upungufu wa chakula duniani,huku watu bilioni 2 wakikabiliwa na tatizo
la lishe na chakula bora wakati bilioni 7 wakiwa katika hatari ya
kushambuliwa na utapia mlo duniani Afrika ikiongoza.
Sorce: Mwananchi
Sorce: Mwananchi