Chelsea
ilitoka nyuma kwa 1-0 na kupata ushindi huo, baada ya makosa ya beki
David Luiz kumpa Jordon Mutch nafasi ya kumfunga Petr Cech, ambayleo
amecheza mechi yake ya 300 Ligi Kuu.
Bao
la kusawazisha la Chelsea lilitokana na maamuzi ya kimakosa ya refa
Anthony Taylorambalo lilifungwa na Edin Hazard dakika ya 34 ambaye
alifunga tena dakika ya 82. Mabao mengine ya The Blues iliyempoteza
kocha wake Mourinho aliyepandishwa jukwaani yalifungwa na Eto’o dakika
ya 66 na Oscar dakika ya 78.
Kikosi
cha Chlesea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Terry, Luiz, Bertrand/Torres
dk64, Ramires, Lampard, Mata/Oscar dk59, WiIlian, Hazard na
Eto’o/Azpilicueta dk69.
Cardiff:
Marshall, Theophile-Catherine, Caulker, Turner, Taylor, Cowie,
Gunnarsson/Gestede dk81, Medel/Kim dk56, Whittingham, Mutch,
Odemwingie/Campbell dk68.
Maajabu: Jose Mourinho alipandishwa jukwaani
Katika
mchezo mwingine mabingwa watetezi, Manchester United wamelazimishwa
sare ya 1-1 Southampton baada ya kuongoza hadi dakika ya 89 Dejan Lovren
alipowapokonya tonge mdomoni Uwanja wa Old Trafford.
Kikosi
cha David Moyes kilipata bao la kuongoza dakika ya 26 mfungaji Robin
van Persie.Kikosi cha Manchester United: De Gea, Rafael, Jones, Evans,
Evra, Carrick, Fellaini/Welbeck dk76, Nani/Giggs dk69, Rooney/Smalling
dk87, Januzaj na van Persie.
Southampton:
Boruc, Clyne, Fonte, Lovren, Shaw, Schneiderlin, Wanyama/Do Prado k83,
Lallana, Steven Davis/Ward-Prowse dk67, Rodriguez/Lambert dk56,
Osvaldo.
Wa,eshindwa kulinda ushindi: Van Persie akishangilia bao lake kwa kumrukia Michael Carrick
Wakachomoa: Dejan Lovren alisawazisha dakika ya 89