Polisi
wa Misri wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuvunja maandamano mjini
Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga mkono rais wa zamani, Mohamed Morsi.
Mawe
yalirushwa na pande zote mbili huku wanafunzi mia kadha wakijaribu
kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa, pahala pa kambi ya wafuasi wa
Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi miwili iliyopita.
Hii
ni siku ya pili ya mapambano katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako
kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.