Home » » HUYU NDIE MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI ANGOLA AMBAYE AMEBADILISHA JINSIA NA KUWA MWANAMKE...

HUYU NDIE MWANAMUZIKI MAARUFU NCHINI ANGOLA AMBAYE AMEBADILISHA JINSIA NA KUWA MWANAMKE...

Mwanamke huyu  kwa jina akijulikana kama Titica, amekuwa ni gumzo kubwa nchini Angola. Siku chache zilizopita UNAIDS ilimpa heshima mwanamke huyu aliyejibadili jinsia kuwa Balozi wake.

Alizaliwa Luanda kama Teca Miguel Garcia, akiwa muimbaji na mchezaji, Titica alibadili 
maumbile yake miaka minne iliyopita mara baaada kufanya upasuaji wa maziwa 
nchini Brazil.Sasa, akiwa na miaka 26, Titica amekuwa kioo cha Angola kwa aina ya muziki anaoufanya wenye mchanganyiko wa miondoko ya rap na techno unaojulikana kama “kuduro”.

Akiongea na BBC mwaka jana, akiwa kwenye kwenye utengenezwaji wa video ya wimbo wake unaotamba sasa uitwao Olha o Boneco, wimbo ambao amemshirikisha muimbaji mashuhuri wa muziki aina ya kizomba aitwaye Ary, Titica alisema amefanikiwa kukabiliana na vikwazo vyake.

“Shukrani kwa Mungu, nina furaha sana, imechukua muda kufika hapa na imehusisha mambo mengi ya kujitolea ila asante Mungu, kila kitu kinakwenda sawa kwangu. Nilikuwa nikipigwa mawe, nimekuwa nikipigwa na kumekuwa na vikwazo vingi vya kisheria dhidi yangu, watu wengi walionyesha hilo. Kuna miiko 
mingi sana,”.

Licha ya miiko hiyo, bado Titica anaonekana kuwa hana upungufu wa mashabiki huku wengi wakiwa wanavutiwa zaidi na muziki wake kuliko jinsia yake.
 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. BONGONEWS TZ - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger