Madereva wa malori zaidi ya mia tatu wamegoma kuendelea na safari katika barabara kuu itokayo Dodoma hadi Mwanza baada ya dereva mwezao aliyekuwa akiendesha lori kuvamiwa na majambazi katika eneo la kisaki manispaa ya Singida.
Wakiongea na ITV /Radio one madereva ambao
wamekutwa katika eneo hilo wameomba jeshi la polisi kufanya doria mara
kwa mara eneo hilo kwani kumekuwa na matuki yanayo jirudia ya utekeji
wa magari kwa kuweka mawe makubwa barabarani na kuwajeruhi madereva
jambo ambalo lina tishia amani kwa watumiaji wa barabara.
Madereva wa malori baada ya kufunga barabara naibu
waziri wa Afrika mashariki Dr. Abdulla Abdulla alikumbwa na adha hiyo na
kusema ni haki ya kikatiba kwa madereva kugoma kwa kudai haki zao,
kutokana na hali hiyo amewahaidi madereva kupeleka kilio chao katika
mamlaka husika ili kuweza kutatua tatizo lao na kukomesha vitendo vya
uvamizi wa magari katika eneo hilo .
Kwa upande wake kamanda wa jeshi la polisi mkoani
Singida SACP Geofrey Kamwela amesema madereva waliamua kusimama
barabarani bila sababu yeyote kwa muda wa zaidi ya masaa matatu na
kusababisha foleni kubwa ambapo kwamujibu wa sheria za usalama
barabarani walikuwa wamefanya kosa ,lakini baada ya viongozi kufika na
kuwasikiliza waliamua kuendelea na safari.
Naye dereva wa lori bwana Agustino Mbawala aliye
tekwa, akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida akiongea kwa
shida huku akiwa na maumivu makali amesema aliona mawe makubwa
barabarani na kuamua kusimama na kukimbia lakini wali mvamia na kumpiga
hatimaye kumpora fedha na simu.
>>ITV
>>ITV