Mama
mmoja amepigwa risasi na polisi kujeruhiwa vibaya maeneo ya mapato
arusha.chanzo cha tukio hilo kinasema kwamba mama huyo alifika maeneo
hayo na kupaki gari yake akitaka kuingia bank lakini akaambiwa eneo hilo
halifai kupaki gari,Mama huyo alipaki gari na kuingia bank alipotoka
alikuta gari lake limetolewa upepo na ndipo vurugu ilianzaa baina yake
yeye na polisi.Vurugu ilipokuwa kubwa mama huyo aliwaambia polisi kwamba
wasimtishie bunduki hata yeye anayo na alipotaka kuitoa polisi
wakampiga risasi.Mama huyo ni muuzaji maarufu wa madini jijini
arusha.Mama huyo amekimbizwa hospitali na yupo chumba cha upasuaji.CHANZO CLOUDS FM