KUNDI
la Jakaya Arts Group limepata pigo tena baada ya kumpoteza msanii
mwenzao wiki mbili zilizopita ambapo kifo kimemchukua msanii mwingine
ambaye ni Pili Ramadhani ‘Awena’ (33) aliyekuwa akiishi Ubungo-Kibangu
jijini Dar es Salaam.
Msanii
huyo alifariki Jumanne wiki hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
baada ya kusumbuliwa na uvimbe kwenye utumbo. Uvimbe huo ulisababishwa
na upasuaji ambao ulipelekea ujauzito aliokuwanao kuharibika ndipo
aliporudishwa tena hospitali kwa ajili ya kusafishwa.
Kwa
mujibu wa ndugu wa familia hiyo aliyefahamika kwa jina la Omari, mwili
wa marehemu ulisafirishwa kwenda kuzikwa kwao Morogoro.
Awena
ameacha watoto wanne, watatu wa kike na mmoja wa kiume. Miongoni mwa
muvi alizocheza ni pamoja na ‘Family Mistake’ ambayo iko katika foleni
ya kutoka na pia alicheza muvi mpya ya RJ inayoitwa ‘Bad Luck’.
CREDIT: GPL