Wanaoenda
huko nje sababu ya kufanya shopping ni uongo mtupu maana ...(akataja
jina la msanii mkubwa wa kike) alishawahi kwenda huko tena alienda kwa
ajili ya kigogo mmoja hapa nchini ambaye alitaka wakutane huko Dubai kwa
ajili ya mapenzi ndipo akapata fulsa ya kufanya na shopping baada ya
kupewa pesa na kigogo huyo" Alisema rafiki huyo
kama kawaida ilitaka kujua ukweli mzima upoje inakuwaje wanaenda nje
kufanya hizo shopping na ni kwa kipato gani wanachopata maana kila siku
wanalia kuwa wasanii maisha ni magumu sasa inakuwaje wanaweza kwenda nje
ya nchi kufanya matanuzi tu?? rafiki huyo alifunguka na kusema tena "Ulishawahi
kumuona msaniii gani wa kiume kaenda kufanya shopping nje ya nchi??
jibu ni hakuna na wao ndiyo wanapata pesa nyingi sana kuliko hao wa
kike. wasanii wa kike wengi wao wanajiuza kwa vigogo ndiyo maana
wanapata hiyo jeuri ya kufanya matanuzi hayo nje ya nchi"
crew yetu ilizidi kumuuliza rafiki huyu wa msanii mkubwa hapa tz kuhusu hilo swala naye bila hiyana aliendelea kufunguka "Hapa
bongo kuna vigogo wakubwa sana wenye pesa zao sasa huwa wanatafuta
wasanii wakike wenye tamaa kwa ajili ya kwenda kufanya nao mapenzi ila
vigogo hao wanaogopa sana mapapalazi kwahiyo huwa wanawachukulia kila
kitu kuanzia usafiri pamoja na malazi katika nchi watayofikia na lengo
likiwa ni kufanya mapenzi tu"
Ilibidi
tumtafute msanii wa kike ambaye anaweza kufunguka juu ya suala hili
ndipo tulipompata Snura na hivi ndivyo alivyofunguka baada ya kumuuliza "Ni kweli wasanii wengi wa kike wanatabia hiyo na wengi wao wanajiuza kweli, ninawafahamu kadhaa ila siwezi kuwataja" alimaliza snura kwa kusema hayo