Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa Khamis M. Mgeja akimpa pole Afisa Mtendaji wa kata ya Ubagwe
katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu Alphonce John Kimario
aliyejeruhiwa kwa kushambuliwa na mapanga na watu aliowataja kuwa ni
wafuasi wa CHADEMA, kupitia vurugu zilizotokea juzi saa moja usiku
katika kata ya Ubagwe muda mfupi baada ya kumalizika kwa kampeni za
kumnadi mgombea wao Bw. Hamisi Majogolo, katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Itabola A.
kizungumza
na waandishi wa habari Afisa huyo Mtendaji wa kata ya Ubagwe, Alphonce
John Kimario amesimulia kuwa sanjari na kuumia vibaya machoni hasa jicho
lake la kulia pia analalamika juu ya maumivu makali anayo yasikia
mgongoni mara baada ya kupigwa na nondo ambapo kwa hivi sasa upande wa
kulia sanjari na bega lake umekufa ganzi.
Ndugu
Alphonce Kimario (Afisa Mtendaji wa kata ya Ubagwe) ambaye amepigwa
nondo, amepigwa mapanga kwenye paji la uso kiasi cha kushonwa nyuzi
kadhaa na kutobolewa jicho moja amekimbizwa hospitali ya Rufaa Bugando
kutokana na hali yeke kuwa mbaya zaidi.
Tabitha
Shuli ambaye ni Afisa Muuguzi Idara ya Macho Hospitali ya Rufaa Bugando
mkoani Mwanza akimhudumia Ndugu Alphonce Kimario.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis M. Mgeja akiongozana na makada wengine
wa CCM mkoa wa Mwanza kuelekea ward nyingine kuwaona majeruhi wengine
walio lazwa katika hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza mara baada
ya kushambuliwa kwa mapanga pamoja na kuharibiwa mali zao mara baada ya
kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wilayani Kahama mkoani
Shinyanga..
Dereva
wa gari la CCM wilaya ya Kahama Charles Peter akiwa katika Hospitali ya
Rufaa ya Bugando kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa mapanga
wakati wa kampeni za udiwani wilayani humo.
Majeruhi
wengine kama Masoud Melimeli (katibu Mwenezi wa Wilaya) amebaki katika
uangalizi wa Hospitali ya Wilaya akiwa na majeruhi wengine kama
Ramadhani Salum (Umoja wa Vijana) na Mussa Daudi (Katibu Uchumi Kata ya
Nyihogo) ambaye alilazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama na mara
baada ya kuzidiwa leo asubuhi amepakiwa katika AMBULANCE kuwahishwa
Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi. Ikitajwa kuwa yeye alipigwa nondo
ya kifuani.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa Khamis M. Mgeja akimpa pole Sebastian Masonga (Katibu UVCCM Kata
ya Majengo) aliyepigwa nondo na hatimaye kuvunjwa mkono wa kushoto,
kuliani ni mwenyeji wa msafara huo ulio tembelea hospitali hiyo, Katibu
wa CCM mkoa wa Mwanza Mama Joyce Masunga.
Sebastian Masonga ambaye ni Katibu UVCCM Kata ya Majengo akisimulia juu ya tukio zima la kuvamiwa.
Pamoja na kulaani vurugu hizo Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halm