Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza kutoa fomu za uchaguzi
mdogo Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa huku kikijinadi kuibuka na ushindi
kwenye uchaguzi huo utakaofanyika Machi 16.
Uchaguzi
huo unafanyika ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa
jimbo hilo, Dk William Mgimwa aliyefariki dunia Januari Mosi, mwaka huu
Hospitali ya Kloof Medi-Clinic nchini Afrika Kusini alikokwenda kwa
matibabu ya figo.
Mkurugenzi
wa Mafunzo na Oganaizesheni wa Chadema, Kigaila Benson alisema fomu
zimenza kutolewa kuanza Februari 5 na kazi hiyo itasitishwa Februari 9,
saa 10:00 jioni.
Benson
alisema upigaji kura za maoni utafanyika Februari 10 mwaka huu, siku
itakayofuata Kamati ya Utendaji ya Jimbo itapitia maoni yaliyotolewa na
kura za maoni kisha itapeleka Kamati Kuu ya Chama yenye jukumu la
kumteua mgombea.
“Febriari
12 mwaka huu, Kamati Kuu itakutana na siku hiyo tutamtangaza mtu ambaye
atapeperusha bendera ya chama chetu, siku tutakayozindua kampeni na
bajeti nzima itakayotumika,” alisema.
Mwananchi