Mtoto Elifrida Nicholaus baada ya kuchomwa moto na shangazi yake.
Akielezea jinsi ilivyokuwa, Elifrida ambaye kwa sasa analelewa katika kituo cha watoto waliofanyiwa ukatili cha Foundation alisema kwa uchungu:
“Nakumbuka siku hiyo shangazi alinifunga mikono na miguu kwa kamba na kuuzungushia mkono wake kipande cha godoro na kunifunga kwa ‘nailoni’ kisha akaniwasha moto mpaka moto ulipoisha, alinichia baada ya mimi kupiga makelele ya maumivu.”
Mkono wa Elifrida Nicholaus baada ya kuunguzwa.
Akizungumza na waandishi wetu, mama wa Elifrida aliyejitambulisha kwa jina la Malina Fabian alisema anaomba msaada wa kisheria kwa kuwa kesi ya mtoto wake inachukua muda mrefu.
‘’Naomba jamani taasisi inayohusika na sheria ishughulikie kesi ya mtoto wangu kuharakisha maana ni muda mrefu sasa,’’ alisema mama wa mtoto huyo.
Awali, kesi ya mtoto huyo ilitakiwa kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mwishoni mwa mwaka jana lakini ilisemekana haikutajwa kutokana na sababu zisizofahamika ndipo tume ya haki za binadamu ilipoingilia kati kwa ajili ya kusikilizwa upya mahakamani hapo. -GPL