Mwanamuziki Ferooz Mrisho akiwa mikononi mwa polisi baada ya kunaswa akivuta bangi.
Habari
zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda na baadaye kuthibitishwa na gazeti
hili, zilisema Ferooz alikuwa akivuta bangi katika eneo hilo kabla ya
majirani wanaokerwa na tabia hiyo, kupiga simu polisi wakitaka
kukomeshwa kwa jambo hilo.
“Hapana
tumechoka na tabia zao, kila ukipita hapa unakula ‘marashi’ ya bangi
tu, vilevile sisi tuna vijana wa rika lao, hawa vijana wanaopita hapa
wanasoma, tunaogopa sana wasije wakajiunga na wao hapa kula ganja,”
alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Ferooz akiwa amepigwa pingu na mwenzake.
Ilidaiwa
kuwa msanii huyo pamoja na wenzake wamekuwa na kawaida ya kukaa katika
kijiwe hicho kila siku na kuvuta bangi huku baadhi yao wakitumia madawa
ya kulevya.
Baada
ya kutiwa nguvuni kwa vijana hao, wakazi wa maeneo hayo wamewamwagia
sifa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini aliyefahamika kwa jina moja la
Mapunda kwa jinsi alivyofanikisha askari kuwahi eneo hilo la tukio.
...Akishushwa kutoka kwenye gari.
“Tulipopiga
simu polisi, hatukutegemea kama ingekuwa haraka hivyo, tunashangaa
baada ya muda mfupi, wakaja eneo hili, kwa kweli huyu mkuu ni mfano wa
kuigwa, maana siku hizi likitokea tukio lolote lile ni dakika chache
gari limefika,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.
Ferooz,
mkali wa kibao cha Starehe baada ya kufikishwa kituoni hapo
alichukuliwa maelezo yake kabla ya kuwekwa rumande. Hadi gazeti hili
likienda mitamboni haikufahamika siku ya kufikishwa mahakamani kwa
wahalifu hao